Wakipewa tu! Hivi hapa viwanja vitano vya Kombe la Dunia Morocco

RABAT, MOROCCO. KATIKA kongamano la 73 la FIFA linalomalizika leo kule Kigali, Rwanda mataifa mbali mbali yalikuwa na nafasi ya kuomba uenyeji wa kmuandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2026.

Afrika ilikuwa inawakilishwa na Morocco na Misri ambazo zimeomba uenyeji lakini Misri imeomba kwa kushirikiana na Saud Arabia na Ugiriki wakati Morocco iliomba kuandaa yenyewe kisha ilipokataliwa ikaungana na Hispania na Ureno kwenye kuandaa kwa pamoja.
Nchi hizo zote zipo karibu karibu na watalaamu  wa mambo wanadai kwamba kuna uwezekano mkubwa nchi hizo tatu zikashinda na michuano hiyo kufanyika Afrika baada ya mara mwisho mwaka 2010.

Kwenye mchakato huo wa kuandaa Morocco iliwasilisha pia na viwanja vitakavyotumika. Sasa hapa tumekuchambulia viwanja vitano vya Morocco vinavyoweza kutumika ikiwa taifa hilo litashinda kwenye mchakato wa uandaaji wa michuano hiyo ya mwaka 2030.


5. Grand Stade de Casablancadagger
Huu ni uwanja mpya unaojengwa pale Jijini Casablanca ambao utakuwa ndio uwanja mkubwa zaidi nchini Morocco ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 93,000.
Ulianza kujengwa rasmi mwaka 2019 na unatarajiwa kufunguliwa mwaka 2015 na gharama za ujenzi ni zaidi ya Bilioni 450 kwa pesa za kibongo na unatarajiwa kufunguliwa mwaka 2025.
Kwa mara ya kwanza mpango ulikuwa ni mechi hizo kutumnika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2026 ikiwa ingepatikana nafasi ya kuiandaa.


4. Ibn Batouta Stadiumdagger
Ni mmoja kati ya viwanja vikubwa sana nchini Morocco. Hiki hakijumuishi soka tu, bali hutumika kwa ajili ya mashindano ya mbio, kuruka viunzi na urushaji tufe.
Gharama za matengenezo yake inakadiriwa kufikia Bilioni 200 kwa pesa za Kitanzania.
Kwa mara ya kwanza ulifunguliwa April 26, 2011 na unaingiza mashabiki 65,000.
Uwanja huu ambao upo karibu na Jijini Tangier ambapo ni karibu kabisa na Hispania umekuwa ukitumika kwenye mechi mbali mbali za mwanzoni mwa msimu za La Liga na Ufaransa.
mwaka 2018  uliandaa mechi kati ya Barcelona na Sevilla ikiwa ni ya ufunguzi wa La Liga ambayo kwa pale England hujulikana kama Community Shield inayokutanisha bingwa wa ligi na bingwa wa kombe la FA.
Mwaka 2018 kwenye michuano ya AFCON uwanja huu ulitumika kwenye mechi sita  za hatua ya makundi na moja ya robo fainali.


3. Marrakesh Stadiumdagger
Ulifunguliwa rasmi mwaka January, 2012, una uwezo wa kuingiza mashabiki 45,240, una uwezo wa kuandaa michezo mbali mbali ukiondoa soka na mwaka 2014 ulitumika kuandaa 2014 IAAF Continental Cup yaliyojumuisha mbio fupi, pia mwaka huo huo ukatumika kuandaa michuano ya Kombe la Dunia kwa upande klabu.
Kuna jumla ya milango 16 ya kuingilia na baada ya kutengenezwa watu wengi waliukosoa kwa sababu eneo la kukimbilia na kuchezea michezo mbali mbali ni kubwa hali inayosababisha mashabiki waingie wachache. Uwanja huu hupo kwenye Jiji la Marrakech.


2. Prince Moulay Abdellah Stadium
Ni uwanja ambao unatumiwa na timu ya jeshi la Morocco ASFAR. Upo kwenye mji mkuu wa nchi hii Rabat. Ulitumika kwenye kuandaa michuano ya Kombe la Dunia kwa upande wa klabu mwaka 2014.
Pia ulijumuishwa kwenye orodha ya viwanja ambavyo vingetumika kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2026 ikiwa Morocco ingeshinda uenyeji.
Kwa mara ya kwanza ulifunguliwa 1983 na una uwezo wa kuingiza mashabiki 45,800. Mbali ya kutumiwa na ASFAR uwanja huu pia unatumika kwenye mazoezi na mechi za kirafiki za timu za taifa za Morocco kuanzia zile za Wanaume na Wanawake.


1. Adrar Stadium
Ni uwanja ambapo katika Jiji la Agadir, uliwahi kutumika kwa michezo minne ya michuano ya Kombe la Dunia kwa upande wa klabu mwaka 2013.Kuanzia
Mwaka 2015 ulikuwa ni mmoja kati ya viwanja vilivyopangwa kutumika kwa ajili ya michuano ya AFCON kabla ya Morocco kusitisha mpango wa kuandaa  michuano hiyo kutokana na kuibuka kwa ugonjwa wa Ebola.
Uwanja huu una uwezo wa kuingiza mashabiki wasiopungu 45,480 na Morocco iliujumuisha kwenye maombi yao ya kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2026 lakini hawakuchaguliwa.
Kwa mara ya kwanza uwanja huu ulitengenezwa mwaka 2004 na ukafunguliwa rasmi mwaka 2010 ambapo Morocco ilikuwa imepanga kuutumia kwa ajili ya Kombe la Dunia ikiwa wangechaguliwa kuandaa michuano hiyo baada ya kuwasilisha maombi yao.