Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waarabu wajiandaa kwa Mohamed Salah

Tetesi Pict
Tetesi Pict

Muktasari:

  • Hadi sasa Liverpool haijaanza kufanya mazungumzo na wawakilishi wa staa huyu na hivi karibuni Salah mwenyewe alithibitisha kuwa ana asilimia nyingi za kuondoka kuliko kubaki.

WINGA wa Liverpool na Misri, Mohamed Salah, 32, bado anahitajika na mabosi wa Saudi Arabia ambao wana ndoto ya kumsajili mwisho wa msimu huu pale mkataba wake utakapomalizika.

Hadi sasa Liverpool haijaanza kufanya mazungumzo na wawakilishi wa staa huyu na hivi karibuni Salah mwenyewe alithibitisha kuwa ana asilimia nyingi za kuondoka kuliko kubaki.

Salah mwenye umri wa miaka 32, tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 19 za michuano yote na kufunga mabao 12.

Kwa sasa ndiye mchezaji anayeongoza zaidi kwa kuhusika kwenye mabao mengi ndani ya EPL ambapo amehusika katika mabao 16 kwa asisti zake sita na mabao 10.


Wakati huo huo Manchester United inajiandaa kulipa Pauni 50 milioni kwenda Benfica kwa ajili ya kumsajili beki wa timu hiyo na Ureno, Tomas Araujo, 22, ambaye pia anawindwa na Chelsea.

Araujo ameonyesha kiwango bora na inadaiwa kuwa ndio pendekezo la kocha mpya Ruben Amorim ambaye anamfahamu vizuri staa huyo.


MANCHESTER City na Manchester United zimepewa nafasi ya kumsajili kiungo wa Juventus na Brazil, Douglas Luiz, 26, katika dirisha lijalo.

Mbali ya Luiz pia Juventus ipo tayari kumuuza kiungo wake raia wa Italia, Nicolo Fagioli, 23.


Timu hizi zimepewa nafasi ya kusajili mastaa hawa baada ya kufanya mawasiliano na mawakala wao.


KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca amekanusha taarifa za kuwa straika wao raia wa Ufaransa, Christopher Nkunku anauzwa na amesisitiza kuwa staa huyo bado yupo katika mipango yao.

Nkunku mwenye umri wa miaka 27, anahusishwa kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza. Mkataba wa Nkunku unamalizika mwaka 2029.


KIUNGO mshambuliaji wa Newcastle United na Paraguay, Miguel Almiron, 30, anaweza kuruhusiwa kuondoka katika dirisha la majira ya baridi mwakani.

Almiron ambaye msimu huu amecheza mechi 14 za michuano yote, anataka kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.


MANCHESTER City inamfuatilia kwa karibu kiungo wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani, Rocco Reitz kwa ajili ya kumsajili katika dirisha la majira ya baridi mwakani. Rocco ana miaka 22.


DHAMIRA kuu ya Barcelona katika dirisha la majira ya kiangazi mwakani ni kusajili winga wa kushoto na Rafael Leao wa AC Milan ndiye chaguo la kwanza, ambaye chini ya Hansi Flick anaelezwa atakuwa bora zaidi.