Verstappen akiri mambo magumu F1

Muktasari:
- Kitendo cha Verstappen kushindwa kushinda angalau mbio mojawapo katika nne zilizopita, zimemfanya aone hatari iliyopo kwake na kampuni yake Red Bull kuchukua tena taji la mbio hizo msimu huu kama mambo yataendelea kuwa yalivyo.
LICHA ya kuongoza kwenye orodha ya alama za ubingwa wa mbio za magari duniani msimu huu, dereva Max Verstappen wa Red Bull amekiri ugumu mkubwa uliopo kwa Sasa kwenye mbio hizo tofauti na matarajio yake.
Kitendo cha Verstappen kushindwa kushinda angalau mbio mojawapo katika nne zilizopita, zimemfanya aone hatari iliyopo kwake na kampuni yake Red Bull kuchukua tena taji la mbio hizo msimu huu kama mambo yataendelea kuwa yalivyo.
Verstappen kuthibitisha kutopendezwa na matokeo ya mbio nne zilizopita, alisema shida inawakabili kwenye gari za Red Bull hazina kasi tena na itazifanya McLaren na Mercedes kufanya vyema mbele yao kwenye mbio zinazokuja mwishoni mwa mwezi huu.
Bingwa huyo mara tatu wa mbio za magari, anatishika zaidi na urejeo mpya wa Lewis Hamilton wa Mercedes ambaye kushinda kwake mbio mbili mfululizo zilizopita, zimemwongezea ari ya kupambana zaidi katika mbio zilizobaki na lolote linaweza kutokea.