Tatum amtisha kocha Warriors

Muktasari:
- Kerr ambaye ni Kocha wa warriors aliyeweka rekodi ya kushinda taji la NBA kama mchezaji na Kocha, ametishika na Celtics pindi atakapokutana nao kwenye mechi za ligi kutokana na kile kilichotokea kwa staa wao Jayson Tatum kwenye michuano ya olimpiki nchini Ufaransa.
WAKATI tukiwa na mwezi mmoja pekee kabla ya kuanza kwa ligi ndefu (regular season) mwezi ujao, Kocha wa timu ya Golden State Warriors, Steve Kerr ameingia ubaridi wa kucheza dhidi ya bingwa mtetezi, Boston Celtics.
Kerr ambaye ni Kocha wa warriors aliyeweka rekodi ya kushinda taji la NBA kama mchezaji na Kocha, ametishika na Celtics pindi atakapokutana nao kwenye mechi za ligi kutokana na kile kilichotokea kwa staa wao Jayson Tatum kwenye michuano ya olimpiki nchini Ufaransa.
Tatum licha ya kuwa na msimu bora na hata kubeba taji la NBA msimu uliopita, alikua na wakati mgumu kupenya kwenye mechi za Marekani katika olimpiki kwani hakupewa nafasi kubwa au dakika nyingi za kucheza mbele ya mastaa wengine.
Hii ni moja, pili ni kitendo cha Kocha huyo kutomjumuisha kabisa staa wao mwinginez Jaylen Brown ambaye ndio aliibuka MVP wa fainali zote mbili za Mashariki na Ile ya NBA mbele ya Dallas Mavericks.
Kocha huyo anaamini atakua na wakati mgumu pindi atakapoenda mbele ya mashabiki wa timu hiyo ambao ni kama hawakupendezwa na maamuzi yake juu ya mastaa wao wote wawili kutomuita mmoja na kutomtumia ipasavyo mmojawapo.