Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot awasilisha jina la De Jong kwa mabosi Liverpool

Muktasari:

  • De Jong ambaye ana umri wa miaka 27, amependekezwa na Arne Slot ambaye anahitaji maboresho katika eneo lao la kiungo.

KIUNGO wa Barcelona na Uholanzi, Frenkie de Jong, 27,  anaweza akajiunga na Liverpool katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

De Jong ambaye ana umri wa miaka 27, amependekezwa na Arne Slot ambaye anahitaji maboresho katika eneo lao la kiungo.

Msimu huu hajapata nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Barca na alianza msimu akiwa na majeraha na hata baada ya kupona amekuwa akiingizwa akitokea benchi.

Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2026 na hadi sasa hakuna dalili za kumwongeza ikielezwa mchakato unakwamishwa na hali ya uchumi ya Barca.

Slot anaamini Liverpool inakosa mastaa kama Jordan Henderson na Fabinho katika eneo lao la kiungo jambo linalochngia kutofanya vizuri.

Hadi staa huyu  amecheza mechi tano za michuano yote  na hajafunga bao wala kutoa asisti.


Jeremie Frimpong

LIVERPOOL inataka kumsajili beki wa  Bayer Leverkusen na Uholanzi, Jeremie Frimpong, 23, katika dirisha la majira ya kiangazi mwakani kwa ajili ya kuziba pengo la Trent Alexander-Arnold, 26, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu na hadi sasa hawajafikia makubaliano ya kumuongeza. Mkataba wa sasa wa Frimpong unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na Kocha Slot anataka kuimarisha kikosi chake msimu ujao.


Milos Kerkez

BEKI wa Bournemouth, Milos Kerkez, 21, huenda akatua Manchester United au Liverpool dirisha lijalo la majira ya kiangazi na sasa timu hizo zote zinapambana kuhakikisha zinampata. Milos mwenye umri wa miaka 21, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza  mechi 12 za michuano yote na kuonyesha kiwango bora kilichozishawishi miamba hiyo ya EPL.


Liam Delap

CHELSEA ipo katika hatua nzuri kwenye mchakato wa kumsajili nyota wa Ipswich Town na England, Liam Delap, katika dirisha lijalo lakini inakumbana na upinzani wa kutosha kutoka kwa Manchester City ambayo pia inazungumza na wawakilishi wake. Delap ni mmoja kati ya mastaa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Ipswich na msimu huu amefunga mabao sita katika mechi 13 za michuano yote.


Ederson

MANCHESTER United, Manchester City na Liverpool zote zipo katika vita kali ya kuiwania saini ya kiungo wa Atalanta na Brazil, Ederson inayehitaji kumsajili katika dirisha lijalo la Januari. Hata hivyo, ripoti mbalimbali zinaeleza kwamba timu itakayofanikiwa kuipata saini yake ni ile itakayotoa zaidi ya Pauni 60 milioni. Mkataba wale unamalizika mwaka 2027 na kuna kila dalili akaenda kucheza England msimu ujao.


Jakub Kiwior

FIORENTINA na Napoli zinataka kumsajili beki wa Arsenal, Jakob Kiwior katika dirisha lijalo kwa mkataba wa mkopo wa nusu msimu lakini hadi sasa Mikel Arteta haonekani kuwa tayari kutoa ruhusa ya fundi huyo kuuzwa kwani bado yupo katika mipango yake. Kiwior mwenye umri wa miaka 24, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Igor Jesus

FULHAM imeendelea kupambana kwa kuipata saini ya straika wa Botafogo ya Brazil, Igor Jesus, 23, dirisha hili lakini inakumbana na upinzani mkali kutoka kwa Newcastle United na Nottingham Forest ambazo zinahitaji huduma yake pia. Tangu kuanza kwa msimu huu Igor amecheza mechi 24 za michuano yote, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Joachim Andersen

JUVENTUS imeanza mazungumzo wawakilishi wa Fulham kwa ajili ya kuipata saini ya beki wao, Joachim Andersen dirisha la majira ya baridi mwakani. Staa huyu anadaiwa anaweza akaigharimu Juventus zaidi ya Pauni 30 milioni. Mkataba wa sasa wa Joachim unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.