Sinner freshi tu bila Djokovic, Alcaraz

Muktasari:
- Sinner ambaye ndiye namba moja kwa ubora wa tenisi kwa wanaume, alitinga robo fainali kwenye michuano hiyo kwa ushindi mbele ya Aussie O'Connell kwa seti 6-1, 6-4 na 6-2.
KAMA Jannik Sinner atafanyia kazi kile alichosema baada ya mshangao uliotokea kwa nyota wawili wa tenisi duniani, Carlos Alcaraz na Novak Djokovic kuondolewa mapema kwenye michuano ya wazi ya Marekani (US Open), basi ana kazi nyepesi ya kubeba taji hilo.
Sinner ambaye ndiye namba moja kwa ubora wa tenisi kwa wanaume, alitinga robo fainali kwenye michuano hiyo kwa ushindi mbele ya Aussie O'Connell kwa seti 6-1, 6-4 na 6-2.

Hivi sasa kazi inabaki kwake kutumia vyema kutowepo kwa Alcaraz na Djokovic kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza, huku Novak akitibua rekodi yake Marekani.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Djokovic kuondoshwa mapema zaidi na kabla ya hapo alikipiga kwa miaka 18 na kutotolewa raundi ya tatu kama ilivyotokea mbele ya Alexei Papyrin aliyemtoa nishai Jumamosi iliyopita.