Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Senegal yaachana na Cisse

Muktasari:

  • Cisse ambaye amekuwa akiinoa Senegal tangu 2015, ni mmoja kati ya makocha waliopata mafanikio makubwa akiwa na Senegal, ikiwemo kuiwezesha kushinda taji la Afcon 2021 baada ya kuichapa Misri kwa penalti 4-3.

CHAMA cha Soka Senegal kimetangaza kuachana na Kocha wa timu ya taifa, Aliou Cisse ambaye mkataba wake ulimalizika Agosti, mwaka huu.

 Pape Thiaw (kushoto) anayekaimu ukocha wa Senegal kwa sasa. Kulia Cisse

Cisse ambaye amekuwa akiinoa Senegal tangu 2015, ni mmoja kati ya makocha waliopata mafanikio makubwa akiwa na Senegal, ikiwemo kuiwezesha kushinda taji la Afcon 2021 baada ya kuichapa Misri kwa penalti 4-3.

Kocha wa zamani wa Senegal, Aliou Cisse akitoa maelekezo kwa nahodha wake, Sadio Mane katika moja ya michezo ambayo timu hiyo ilicheza chini ya ukufunzi wake.

Vilevile aliiwezesha kushinda Kombe la CHAN 2022 katika michuano iliyofanyika 2023 nchini Algeria.

Kikosi cha timu ya taifa ya Senegal

Mbali ya kushinda makombe hayo, Cisse pia aliiongoza Senegal kucheza hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2022 kwa mara ya kwanza tangu 2002.

Katika michuano ya Afcon 2019 aliifikisha timu hiyo fainali mara ya kwanza tangu 2002 ingawa ilipoteza mbele ya Algeria kwa bao 1-0.

Cisse (kushoto) wakati akiichezea Senegal miaka ya 15 iliyopita. Picha nyingine akiwa kocha wa timu hiyo

Cisse anaachana na Senegal akiwa ndiye kocha aliyedumu muda mrefu katika nafasi hiyo kuliko yeyote kwenye historia ya taifa hilo.

Taarifa zinaeleza kwamba kwa sasa Pape Thiaw ambaye ni kocha msaidizi atachukua nafasi ya Cisse wakati mchakato wa kutafuta kocha mpya ukiendelea.

Cisse ambaye ana uraia wa Senegal na Ufaransa alianza safari ya ukocha akiwa na Louh-Cuiseaux ya Ufaransa alikodumu kama kocha msaidizi kabla ya kurudi Senegal kufundisha timu za taifa za vijana katika ngazi tofauti na baadaye kupewa mikoba ya kuinoa Senegal kuanzia Machi 2015.