Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Piga ua bingwa NBA yupo hapa

Muktasari:

  • Taji hilo lilikuwa la 18 kwa Celtics ikiweka rekodi ya jumla katika historia ya NBA. Hakuna timu iliyobeba mataji 18 zaidi ya Celtics kuwa ya kwanza kuyafikia na kuwaachia vumbi Los Angeles Lakers ya Magharibi iliyo na mataji 17.

MASHABIKI wanahesabu siku zisizozidi 50 kabla ya kuanza kwa ligi ndefu ya NBA mwezi ujao ambapo ataanza kusakwa bingwa mpya wa msimu wa 2024/25 kufuatia msimu uliopita taji hilo kwenda kwa Boston Celtics ya ukanda wa Mashariki iliyoifunga Dallas Mavericks ya Magharibi.

Taji hilo lilikuwa la 18 kwa Celtics ikiweka rekodi ya jumla katika historia ya NBA. Hakuna timu iliyobeba mataji 18 zaidi ya Celtics kuwa ya kwanza kuyafikia na kuwaachia vumbi Los Angeles Lakers ya Magharibi iliyo na mataji 17.

Hapo ndipo moto utawaka msimu ujao baina ya timu hizo mbili zinazofukuzana kwenye taji, huku pia kukiwa na timu zinazolisaka kwa karibu na zimepewa ‘odds’ za kulibeba  ambazo ni Oklahoma City Thunder yenye +700, Philadelphia 7ers yenye +850, New York Knicks +900 na Celtics inayoongoza kupewa nafasi kubwa ikiwa nazo +295. Zifuatazo ni timu zinazoweza kulibeba taji hilo bila kujali aina ya odds zilizopewa kwenye utabiri.


MINNESOTA TIMBERWOLVES

Licha ya kupewa odds +1000 za timu zinazowekwa kwenye nafasi ya kubeba taji msimu ujao, haimaanishi timu zenye odds ndogo juu yake zina nafasi kubwa zaidi kutokana na ubora na aina ya kikosi kilivyokuwa na ubora msimu jana na hata unaokuja. Anthony Edwards, Rudy Gobert na Karl-Anthony Towns ndiyo wachezaji vinara wanaoiweka kwenye nafasi kubwa Wolves kushinda taji la msimu ujao mbele ya wapinzani wengi.


PHOENIX SUNS

Mara ya mwisho walikaribia kubeba taji hili 2021 walipocheza fainali dhidi ya Milwaukee Bucks na kupoteza, na tangu hapo wamefanya usajili mkubwa wenye lengo la  kulichukua taji bila mafanikio ndani ya miaka mitatu mfululizo. Usajili wa Kevin Durant na Bradley Beal ndani ya mwaka mmoja uliopita umedhihirisha lengo ambapo kikosi cha timu hiyo kina nafasi kubwa ya kubeba taji kikiwa na utatu wa Devin Booker ndani yake.


DENVER NUGGETS

Baada ya kubeba taji 2023, Nuggets inayoongozwa na MVP Nikola Jokic ina nafasi kubwa ya kuchukua taji tena kutokana na kikosi kuwa vilevile na safari hii ameongezeka mkali wa triple-double, Russell Westbrook.


DALLAS MAVERICKS

Hawakupewa nafasi kubwa msimu uliopita kucheza fainali kutokea Magharibi mbele ya Nuggets na Wolves, lakini walishtua kwa kuupiga mwingi na kuiondosha Wolves iliyoivua ubingwa Nuggets na kwenda kukipiga na Celtics  fainali waliyopoteza kwa 4-1. Nyongeza ya Klay Thompson mwenye mataji manne itawaongezea sababu kina Luka Doncic na Kyrie Irving waliokwama mbele ya Celtics.


LAKERS, BUCKS, WARRIORS

Timu hizo tatu pia zina nafasi kubwa ya kushinda taji msimu ujao kutokana na kuwa na wachezaji wenye uwezo wa kufanya makubwa bila kujali nafasi wanayopewa na watabiri.

Lakers ya LeBron, Anthony Davis inasubiriwa kurudia ilichofanya 2020 ilipotwaa taji la 17 huku Bucks ya Giannis Antetokoumpo ikiwa tishio inayoweza kubeba baada ya mara ya mwisho kubeba 2021 ilipoifunga Suns.

Golden State Warriors ilibeba taji mwaka jana ilipoifunga Celtics kwenye fainali licha ya kutohesabiwa na wengi wakati huo kwamba itashinda, lakini ilibeba.

Uwepo wa Steph Curry ni silaha namba moja Warriors kushinda taji kama itakuwa fiti mwanzo mwisho hususan hatua ya mtoano (playoffs).