Norris Vs Max, kazi ipo Formula 1

Muktasari:
- Norris alifanikiwa kumzidi kete Verstappen kwa sekunde 20 kushinda mbio hizo mbele ya Verstappen ambaye alishika nafasi ya pili na kufanya pengo la pointi baina yao liwe 52, Verstappen akiendelea kuwa juu licha ya kufikisha mbio nane mfululizo bila kushinda.
USHINDI WA dereva Lando Norris wa McLaren kwenye mbio zilizopita za Singapore, zilikua muhimu kwake katika jitihada za kushinda taji la mbio za mwaka huu mbele ya bingwa mtetezi, Max Verstappen.
Norris alifanikiwa kumzidi kete Verstappen kwa sekunde 20 kushinda mbio hizo mbele ya Verstappen ambaye alishika nafasi ya pili na kufanya pengo la pointi baina yao liwe 52, Verstappen akiendelea kuwa juu licha ya kufikisha mbio nane mfululizo bila kushinda.
Norris sasa anahitaji kuendelea kushinda mbio sita zilizobaki au kumuombea Verstappen aendelee kutoshinda huku yeye akihitaji kumaliza ndani ya tatu bora (podium) ili kumaliza utawala wa Verstappen aliyechukua taji hilo mara tatu mfululizo.