Norris, Vestappen kazi ipo F1

Muktasari:
- Norris aliibuka mshindi mbele ya Verstappen ambaye sasa amefikisha mbio tano mfululizo bila ushindi, kiasi cha kuweka rehani ubingwa aliochukua mara tatu mfululizo tangu alipomvua Lewis Hamilton.
USHINDI wa dereva Lando Norris wa McLaren kwenye mbio za Uholanzi ambapo ndiko nyumbani kwao Max Verstappen, kumezidisha utamu mwishoni mwa mbio za magari duniani maarufu Formula One ambazo zimebakiza mbio tisa ili kukamilisha msimu.
Norris aliibuka mshindi mbele ya Verstappen ambaye sasa amefikisha mbio tano mfululizo bila ushindi, kiasi cha kuweka rehani ubingwa aliochukua mara tatu mfululizo tangu alipomvua Lewis Hamilton.
Norris amebakiza pointi 70 kumfikia Verstappen kwenye pointi za ubingwa na kama hatashinda mbio mbili zijazo itakuwa habari tofauti kwa Verstappen ambaye ameshaingiwa woga wa kutetea taji hilo.
Verstappen ameshaeleza wasiwasi wake kwa kampuni yake, Red Bull kwamba kuna kitu hakiendi sawa kiasi cha kumuweka pabaya kutetea ubingwa ambao upo rehani kwa kushindwa kuibuka na ushindi katika mbio tano mfululizo.