Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Norris, Verstappen kazi ipo Arzebaijan

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Verstappen ana pointi 303 akiwa ameshinda mbio saba mwaka huu na kuingia tatu bora (podium) mara 10 wakati Norris ameshinda mbio mbili na kuingia podium mara 10 pia wakitafutana vilivyo kwenye kusaka taji hilo ambalo bado halina mwenyewe.

POINTI 62 pekee ndizo zinatenganisha vita ya ubingwa wa mbio za magari kati ya Max Verstappen wa Red Bull na Lando Norris wa McLaren kwenye msimamo wa jumla.

Verstappen ana pointi 303 akiwa ameshinda mbio saba mwaka huu na kuingia tatu bora (podium) mara 10 wakati Norris ameshinda mbio mbili na kuingia podium mara 10 pia wakitafutana vilivyo kwenye kusaka taji hilo ambalo bado halina mwenyewe.

Wikiendi hii mbio zinaenda kufanyika Azerbaijan baada ya kupumzika wikiendi iliyopita na wote wawili walishindwa mbele ya Charles Leclerc wa Ferrari ambaye amesogea kwa kufikisha pointi 217 akiwa ameshinda mbio mbili na kuingia podium mara nane.

Dereva mwingine aliyeshinda mbio mbili mwaka huu mbali na Norris na Leclerc ni Lewis Hamilton wa Mercedes ambaye hata hivyo mwanzo mbaya umemfanya awe mbali kwa pointi 164 na kaingia kwenye podium mara nne pekee.