Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nadal ‘kuitibulia’ Hispania

Muktasari:

  • Wasiwasi juu yake kutoka kwa mashabiki wa tenisi na Hispania kama ataweza kwenda kushiriki michuano hiyo umekuja baada ya bingwa huyo mara 22 wa mataji makubwa (Grand slam) duniani, kulazimika kujitoa kwenye michuano tofauti mwaka huu ikiwemo ya karibuni ya Marekani (US Open)  na Laver Cup.

RAFAEL NADAL wa miaka 38 haaminiki tena mbele ya mashabiki wa tenisi duniani achilia mbali hata wahispania wenzake ambao wameweka shaka juu yake kuelekea hatua ya mtoano ya michuano ya Davis Cup mwezi Novemba.

Wasiwasi juu yake kutoka kwa mashabiki wa tenisi na Hispania kama ataweza kwenda kushiriki michuano hiyo umekuja baada ya bingwa huyo mara 22 wa mataji makubwa (Grand slam) duniani, kulazimika kujitoa kwenye michuano tofauti mwaka huu ikiwemo ya karibuni ya Marekani (US Open)  na Laver Cup.

Sasa shughuli inakuja kwenye hatua ijayo ya Davis ya Novemba kama atashiriki au kujitoa kufuatia kuchaguliwa kuwakilisha taifa hilo akijumjuishwa pamoja na Carlos Alcaraz, Pablo Busta, Roberto Bautista na Marcel Granollers.

Nadal aliyetwaa taji la Davis mara tano wakati akiwa kwenye ubora wake, anatajwa kuwa mbioni kustaafu tenisi wakati wowote baada ya awali kudhaniwa angefanya hivyo baada ya michuano ya olimpiki nchini Ufaransa.