Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayweather Jr kwanini lakini?

Muktasari:

  • Hii ni kufuatia pambano lake lingine la maonyesho lililofanyika wikiendi iliyopita dhidi ya John Gotti III kuwaboa watazamaji zaidi ya 20,000 waliolipa viingilio kuwashuhudia nchini Mexico.

BONDIA anayetajwa kuwa bora kwa muda wote kupitia rekodi zake za ulingoni, Floyd Mayweather Jr ni kama anatakiwa kuchagua moja kati ya kupotezea mapambano anayocheza ya maonyesho au aendelee bila kujali nini watu wanataka.

Hii ni kufuatia pambano lake lingine la maonyesho lililofanyika wikiendi iliyopita dhidi ya John Gotti III kuwaboa watazamaji zaidi ya 20,000 waliolipa viingilio kuwashuhudia nchini Mexico.

Pambano hilo ambalo kama kawaida halikuwa la ushindi wala mkanda wa kushindania zaidi ya kuwa maalumu, liliboa kutokana na kutumia zaidi ya dakika mbili kupumzika kwao kila baada ya raundi moja katika  raundi nane zilizotumika kupiganiwa.

Mbali na wakati mwingine kengele ya kumaliza raundi kutosikika kiasi cha kuboa, pia kuwa la upande mmoja ambao Mayweather Jr alitawala zaidi.

Pambano hilo lilikosa mvuto kiasi cha kuonekana bondia huyo mwenye rekodi ya kucheza mapambano 50 bila kupoteza kuwafanya baadhi ya mashabiki wamshauri aachane tu na mapambano hayo ya maonyesho.