Man United, Villarreal hawajawahi kufungana

Friday May 07 2021
MAN PIC

London, England. Mchezo wa fainali ya Ligi ya Europa utachezwa siku tatu kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakati Villarreal itakapocheza na Manchester United.

Hii inakuwa fainali ya pili ya Europa kwa Manchester United baada ya ile ya 2017, wakati kwa miamba hiyo ya Hispania, Villarreal ni mara yao ya kwanza katika hatua hiyo.

Villarreal imefanikiwa kuondoa kumbukumbu ya kucheza fainali za Ulaya kwa timu nne za England, ambayo ingerudia msimu wa 2018-19, wakati Livepool na Tottenham zilipocheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Villarreal hadi fainali

Villarreal imefanikiwa kutinga fainali ya Ligi ya Europa kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo. Hiyo ni baada ya kutia Arsenal kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.

Villarreal ilianza mbio za fainali katika hatua ya makundi, wakati ikishindi michezo mitano na sare moja. Sare yao ilikuwa dhidi ya Maccabi Tel Aviv, wakati Nyambizi la Njano likiongoza katika kundi lao.

Advertisement

Mara ya mwisho kukutana Ulaya

Man United na Villarreal zimekutana mara nne, katika na Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi ya msimu wa 2005/06 na 2008/09.

Lakini cha zaidi, katika kukutana kote timu hizo hazijawahi kufungana bao hata moja, lakini kulikuwa na vituko zaidi vya uwanjani, kadi nyekundu na pia mipira kugonga nguzo zaidi.

Wachezaji kucheza timu zote

Cha kufurahisha zaidi, timu hizi zimewahi kuuziana wachezaji kwa kipindi kirefu na wachezaji kadhaa wamecheza kwa nyakati tofauti katika vikosi hivi.

Mfano mzuri ni nyota wa sasa wa Manchester United, Eric Bailly, ambaye aliichezea Villarreal msimu wa 2015/16, lakini alisajiliwa na Manchester United 2016 hadi sasa.

Diego Forlán aliichezea Manchester United msimu wa 2002/04, kabla ya kusajiliwa na kuichezea Villarreal 2004 hadi 2007, hilo lilitokea pia kwa Giuseppe Rossi, ambaye aliichezea Manchester United 2004 hadi 2007, kabla ya kutua Villarreal 2007 akidumu hadi 2013.

Antonio Valencia alikuwa mchezaji wa Villarreal kuanzia 2005, hadi aliposajiliwa na Manchester United, ambako alidumu kwa miaka 10, kuanzia 2009 2019.

Advertisement