Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City, Jack Grealish hakijaeleweka

GREALISH Pict

Muktasari:

  • Man City ilimwacha nje ya kikosi nyota huyu ili amakinike zaidi katika kutafuta timu atakayojiunga nayo na tovuti ya GiveMeSport, inaeleza mabosi wa Man City walitarajia hatma yake iwe imeamuliwa kabla ya kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya, lakini hilo linaonekana kuwa gumu zaidi kadri muda unavyosonga.

MANCHESTER, ENGLAND: LICHA ya kutomjumuishwa katika kikosi kilichokwenda kucheza mashindano ya Kombe la Dunia kwa Klabu Marekani, staa wa Manchester City Jack Grealish hadi sasa bado hajapata timu.

Man City ilimwacha nje ya kikosi nyota huyu ili amakinike zaidi katika kutafuta timu atakayojiunga nayo na tovuti ya GiveMeSport, inaeleza mabosi wa Man City walitarajia hatma yake iwe imeamuliwa kabla ya kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya, lakini hilo linaonekana kuwa gumu zaidi kadri muda unavyosonga.

Tatizo kubwa ni kukosekana kwa timu iliyo tayari kutoa ofa ya kuridhisha inayofikia kiasi ambacho Man  City inakihitaji.

Kikosi cha Pep Guardiola kiko tayari kumuuza  Grealish moja kwa moja au kwa mkopo, ili kupata pesa na nafasi ya kusajili wachezaji wengine.

Grealish mwenyewe anaripotiwa kuwa na kipaumbele cha kucheza barani Ulaya ili kujijenga upya ingawa kuna ofa kadhaa kutoka Saudi Arabia.

Kipaumbele kwa Grealish ni kucheza mara kwa mara katika ligi yenye ushindani, ili aweze kupata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England kwa ajili ya Kombe la Dunia lijalo la mwakani, hasa kwa kuwa hajawahi kuitwa tena tangu Thomas Tuchel alipoteuliwa kuwa kocha mkuu wa England.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa Newcastle wamehusishwa kwa muda mrefu na Grealish, lakini hadi sasa hawajawasiliana wala kutoa ofa yoyote rasmi, pia Napoli na AC Milan zinaonyesha nia, lakini zinaonekaa kumweka kama chaguo la pili ikiwa zitakosa mastaa zinaowawinda kwanza.

Kwa sasa, hatma ya Jack Grealish bado haijulikani, huku dirisha la usajili likiendelea kusonga mbele bila ofa thabiti mezani kwa Man City.