Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kanuni ya mchujo itazamwe upya

MCHUJO Pict

Muktasari:

  • Na hapa sio kwa Ligi Kuu tu bali hadi Ligi ya Championship na First League ambayo ni madaraja yanayoongozana katika ngazi ya soka la Tanzania.

WALIOSHAURI na kupitisha kanuni ya kuwepo mechi za mchujo inawezekana walikuwa na nia nzuri lakini baada ya kijiwe kufanya tathmini ya misimu kadhaa ambayo kanuni hiyo imetumika kina ushauri wake.

Na hapa sio kwa Ligi Kuu tu bali hadi Ligi ya Championship na First League ambayo ni madaraja yanayoongozana katika ngazi ya soka la Tanzania.

Kijiwe kinashauri kanuni hiyo iendelee kutumika lakini isihusishe timu za daraja moja dhidi ya daraja jingine kwa vile haitengenezi mazingira ya usawa kimpira na hivyo kufubaisha ushindani ambao unategemewa.

Mfano kwa hivi sasa, timu za Ligi Kuu zilizoshika nafasi ya 13 na 14 zinacheza zenyewe katika mchujo (play off) kupata timu moja ya kubaki kwenye ligi na inayofungwa inacheza na timu inayofanya vizuri kwenye mchujo wa Championship.

Huko Championship timu inayoshika nafasi ya tatu, inacheza dhidi ya timu inayoshika nafasi ya nne kupata timu moja ambayo inakutana na timu iliyoshindwa mchujo katika Ligi Kuu kusaka nafasi moja ya kucheza katika msimu unaofuata wa Ligi Kuu.

Hapa maana yake mchujo unaipa faida timu inayoshindwa mara mbili katika Ligi Kuu kujitetea kwa mara ya tatu lakini jambo kama hilo halifanyiki kwa timu ya Championship ambayo yenyewe inajitetea mara moja tu.

Lakini ikumbukwe Ligi ya Championship huwa inawahi kuisha mapema kabla ya Ligi Kuu hivyo timu inayopata fursa ya Championship inayopata fursa ya kucheza mchujo, inajikuta ikilazimika kukaa kwa muda mrefu bila kucheza mechi za ushindani kusubiri timu ya Ligi Kuu.

Hapo wachezaji wa timu ya Championship wanalazimika kucheza mechi ya mchujo wakiwa wanakosa ufiti wa mechi tofauti na wenzao wa Ligi Kuu ambao muda huo wanakuwa wa moto kwa sababu wanakuwa wametoka katika ushindani.

Hapo sijazungumzia suala la kiuchumi kwa maana ya kwamba udhamini kiduchu wa Championship unaifanya timu ya daraja hilo kupata wakati mgumu kifedha katika maandalizi kulinganisha na mpinzani wao wa Ligi Kuu.