Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamondi, Singida BS ni suala la muda tu!

GAMONDI Pict

Muktasari:

  • Gamondi aliyejiunga na   Yanga Julai 11, 2023 na akachukua ubingwa wa Ligi Kuu na FA, aliondoka  Novemba 15, mwaka jana imeelezwa sababu ya kujiunga na SBS ni uzoefu alionao ambao mabosi wa Singida wanaoamini utawasaidia katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

KUNA taarifa za aliyekuwa kocha wa Yanga, Miguel Gamondi yupo mbioni kujiunga na Singida Black Stars kwa ajili ya kuifundisha msimu ujao.

Gamondi aliyejiunga na   Yanga Julai 11, 2023 na akachukua ubingwa wa Ligi Kuu na FA, aliondoka  Novemba 15, mwaka jana imeelezwa sababu ya kujiunga na SBS ni uzoefu alionao ambao mabosi wa Singida wanaoamini utawasaidia katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Kama uongozi wa SBS ukifanikiwa kupata saini ya Gamondi ataziba pengo la David Ouma aliyeisaidia timu hiyo kufika fainali ya Kombe la FA na kumaliza nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Chanzo cha ndani kutoka timu hiyo Kimesema; "Gamondi alikuwa anahitajika kwa muda mrefu SBS, lakini akachukuliwa kocha Patrick Aussems aliyewahi kuifundisha Simba kwa mafanikio, lakini hatukuweza kumaliza naye msimu.

"Tumefikia hatua nzuri katika mazungumzo yetu, muda wowote anaweza akasaini kwa ajili ya kuifundisha timu msimu ujao ni kocha mzuri tunamtegemea atatusaidia sana katika michuano ya CAF."