Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kane na imani ya mataji Bayern Munich

Kane Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 hajawahi kutwaa taji lolote kubwa katika maisha yake ya soka kuanzia katika ngazi ya klabu hadi timu ya taifa.

MUNICH, UJERUMANI: Harry Kane anaamini kwamba msimu huu atamaliza nuksi ya kutotwaa mataji kwani timu yake Bayern Munich ina kila kigezo cha kumtimizia imani yake.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 hajawahi kutwaa taji lolote kubwa katika maisha yake ya soka kuanzia katika ngazi ya klabu hadi timu ya taifa.

Ilionekana Bayern Munich ingempatia taji la kwanza kubwa msimu uliopita baada ya kujiunga nayo akitokea Tottenham Hotspur kwa dau la Pauni 100 milioni lakini matokeo yake ilikosa ubingwa wa Ligi Kuu ya Ujerumani ambao ulienda kwa Bayer Leverkusen huku taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya likichukuliwa na Real Madris.

Mwaka 2019 alikaribia kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya alipoingia fainali akiwa na Spurs lakini walifungwa mabao 2-0 na Liverpool na mara mbili tofauti alikosa taji la Euro akiwa na timu ya taifa ya England, mwaka 2020 na 2024.

Lakini Kane ameonekana kutokata tamaa na ametamba kuwa atatwaa mataji mengi akiwa na Bayern Munich hivyo hana presha wala wasiwasi wowote.

“Nimekuwa nikisikia swali hili nikiulizwa kila wakati. Ni kweli kwamba hadi sasa nimeshinda tuzo nyingi binafsi kama vile ufungaji bora na mchezaji bora. Lakini huwa naanza kila msimu nikiwa na lengo la kushinda na kukusanya mataji na sijatosheka na kutambulishwa na tuzo binafsi.

“Sasa nakuambia kuwa nina miaka 31. Kwa wakati fulani, katika umri kama huo ulikuwa ni mwanzo wa mwisho. Leo kwa mambo yanavyokwenda, ni kwamba tunafika ubora wetu katika umri wa miaka 30. Na nahisi ubora wa Harry Kane bado haujaja. Nina uhakika na hilo.

“Nina uhakika mkubwa na ukweli kwamba sehemu ya pili ya kazi ndio inayofunguka sasa na nitakuwa tajiri wa mataji,” alitamba Kane.

Kane alisisitiza kuwa anaamini mataji ambayo atatwaa siku za usoni yatamfanya asikutane tena na ukosoaji wa nuksi ya makombe pindi akistaafu soka tofauti na ilivyo hivi sasa.

Mshambuliaji huyo alisema kuwa anaamini hilo halitotokea kwa Bayern Munich pekee bali hata timu ya taifa ya England.

“Ninaona fahari kupitiliza kwa kile nilichokipata lakini ninajua kuhusu hilo. Nahitaji mataji ya kuonyesha,” alisema Kane.

Alisema kuwa pamoja na ukosoaji ambao amekuwa akipata, anajitahidi kuwa na utulivu na kutojiondoa mchezoni na hilo anadhani ndio sababu kubwa inayomfanya aendelee kufanya vizuri.

Katika msimu huu, tayari Kane ameifungia Bayern Munich mabao 21 na timu hiyo inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Ujerumani ikiwa na pointi 39.