Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JOSHUA Vs DUBOIS: Vita ya watoto wa nyumbani

Muktasari:

  • Pambano hilo ni la pili kubwa baada ya lile la mwezi Mei lililowakutanisha Oleksandr Usyk na Tyson Fury waliopigana mjini Riyadh nchini Saudi Arabia, tofauti na hili linalopigwa ndani ya dimba maarufu la soka duniani, Wembley.

SIKU TATU kutoka Leo Jumatano, hatimaye dunia inaenda kushuhudia pambano kubwa la uzito wa juu (heavyweight) linalowakutanisha waingereza Anthony Joshua na Daniel Dubois watakaopanda ulingoni Jumamosi hii uwanjani Wembley mjini London.

Pambano hilo ni la pili kubwa baada ya lile la mwezi Mei lililowakutanisha Oleksandr Usyk na Tyson Fury waliopigana mjini Riyadh nchini Saudi Arabia, tofauti na hili linalopigwa ndani ya dimba maarufu la soka duniani, Wembley.

Dubois ndiye anaingia kama mwenye mkanda wa IBF aliouchukua kwa Oleksandr Usyk aliyelazimika kuuachia bila kupigwa wakati akisubiri kupanda ulingoni kuzichapa na Tyson Fury mwezi Desemba.


MTIFUANO MEZANI, UZITO

Utamu wa pambano hilo unanogeshwa na kile kilichotokea kwenye meza ya duara baina ya mabondia hao mapema mwaka huu ambapo waliliamsha kiasi cha kunusurika kuzichapa ‘kavukavu’ wakiwa na wasimamizi wakijadiliana mipango ya pambano na kuishia kutulizwa kama sio kuamuriwa kutulia.

Ndivyo pia ikawa wakati wa kupima uzito wiki hii jambo ambalo liliongeza upinzani wa pambano hilo la kuvutia ambalo sasa linakwenda kuwa la kutazamwa zaidi kwa kila bondia kutaka kuthibitisha ubabe wake.


MKANDA KUNOGESHA

Tayari Joshua ameshapigana mapambano matatu makubwa nyuma bila kuwania mkanda wowote wa juu wakati ambao Dubois naye amepigana bila kubeba mkanda lakini akafanikiwa kupata haki ya kuuwania mkanda wa IBF mbele ya Usyk ambaye ana mkataba wa kurudiana na Fury hivyo ikamlazimu kuuachia mikononi mwa Dubois.

Hii inamaanisha kwamba, mabondia wote wawili wataenda kuuwania mkanda huo ili kuumiliki na ni hauna mwenyewe kwa sasa hadi kushinda pambano ndipo utakua na tambo za kuushikilia.

Kabla ya hapo, ikumbukwe Joshua alishawahi kuushikilia pamoja na ile mingine ya WBA na WBO kabla ya kuvuliwa na Usyk.


USYK NDANI YA UWANJA

Hili ni jambo lingine linalonogesha pambano hilo kubwa kwa kuwepo Oleksandr Usyk ndani ya uwanja kushuhudia pambano .

Usyk anatarajia kuingia kushuhudia mbabe wa kukutana naye kama atafanikiwa kumchapa tena Tyson Fury, Desemba, hivyo anakeenda kwa lengo la kuwasoma wote wawili kabla ya kuanza mipango ya kuzichapa na atakayeshinda siku hiyo.


MBABE ASUBIRIWA

Pambano hilo kwa kiasi kikubwa limewekewa matarajio ya kumalizika kwa ushindi iwe ndani ya raundi 12 au pungufu ndio sababu kubwa ya wengi kutaka kulitazama ili waone ni bondia yupi atafanikiwa kuushikilia mkanda wa IBF.