Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Greenwood apewa beji maalumu Ufaransa

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa zamani wa Manchester United ameanza kwa moto kwelikweli huko kwenye klabu ya Marseille tangu alipojiunga nayo kwenye dirisha la majira ya kiangazi. Greenwood alijiunga na timu hiyo ya Ufaransa kwa ada ya Pauni 30 milioni, huku Man United ikiweka kipengele cha kupewa asilimia 50 ya pesa zitakazopatikana endapo kama atauzwa.

MARSEILLE, UFARANSA: WINGA matata, Mason Greenwood amekabidhiwa beji maalumu iliyowekwa kwenye jezi zake anavyovaa kwenye mechi za Ligue 1.

Fowadi huyo wa zamani wa Manchester United ameanza kwa moto kwelikweli huko kwenye klabu ya Marseille tangu alipojiunga nayo kwenye dirisha la majira ya kiangazi. Greenwood alijiunga na timu hiyo ya Ufaransa kwa ada ya Pauni 30 milioni, huku Man United ikiweka kipengele cha kupewa asilimia 50 ya pesa zitakazopatikana endapo kama atauzwa.

Greenwood amefunga mabao matano katika mechi zake nne za kwanza, ikiwamo kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya Toulouse kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa. Kwa kasi yake hiyo ya kufunga aliyoanza nayo kwenye Ligue 1, staa huyo alipewa beji maalumu ambayo alivaa Jumamosi iliyopita, wakati Marseille ilipokipiga na Nice.

Greenwood, 22, alivaa beji hiyo inayohusu mfungaji bora baada ya kuongoza kwa mabao kwenye mechi za wikiendi zilizopita. Beji hiyo yenye rangi nyeupe na logo ya dhahabu inaitwa S1 ilitambulishwa rasmi mwanzoni mwa msimu huu.

Hata hivyo, Greenwood alishindwa kutumia vyema siku yake hiyo baada ya kutoka kapa kwa mara ya kwanza msimu huu, wakati timu yake ya Marseille ikishinda 2-0. Licha ya kuanza msimu kwa kasi, kocha wa mpito wa England, Lee Carsley ameweka kando uwezekano wa kumrudisha mkali huyo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England. Kutokana na hilo, Greenwood sasa anafikiria kubadili utaifa achezee Jamaica.