Dubois atamba, aonywa kwa Joshua

Muktasari:
- Hata hivyo, lile la tarehe 20, mwezi huu litahusisha mabondia ambao wote ni Waingereza, Daniel Dubois na Anthony Joshua kwenye Uya uwanja wa Wembley, England, kuamua bondia atakayeshikilia mkanda wa IBF ambao umeachiwa huru na Oleksandr Usyk.
SIKU 10 zimebaki kabla ya dunia kushuhudia pambano lingine kubwa la uzito wa juu duniani (heavyweight) baada ya mwezi Mei kutanguliwa na lile la Oleksandr Usyk na Tyson Fury.
Hata hivyo, lile la tarehe 20, mwezi huu litahusisha mabondia ambao wote ni Waingereza, Daniel Dubois na Anthony Joshua kwenye Uya uwanja wa Wembley, England, kuamua bondia atakayeshikilia mkanda wa IBF ambao umeachiwa huru na Oleksandr Usyk.
Wakati baadhi wakiamini pambano hilo litakua upande wa Joshua ambaye aliwahi kuushikilia mkanda huo na kuupoteza kwa Usyk pamoja na ile mingine ya WBO na WBA, Dubois ameahidi kuwashangaza kwani amejipanga vyema kumchapa Joshua ulingoni na sio mdomoni mwa watu.
Billy Joe Saunders, aliyekua bingwa wa dunia uzito wa middleweight, amekinzana na tambo za Dubois kwa alichokiona kwenye mazoezi ya Joshua, huyu wa sasa ni hatari zaidi ya alivyowahi kuwa na sio yeye (Dubois) tu bali bondia yeyote atakayekutana naye atakua kwenye matatizo.