Docic, AD kumrithi Lebron

Muktasari:
- LeBron ndilo jina kubwa ambalo kwa muda mrefu liko juu kwenye thamani ya kitimu na kwake binafsi, kiasi cha kuifanya Lakers kutazamwa zaidi kote duniani hususan mechi za ligi zinazohusisha timu hiyo.
LICHA ya supastaa wa mpira wa kikapu na timu ya Los Angeles Lakers inayoshiriki Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), LeBron James kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kubaki, nyakati zinakwenda mwishoni kabla ya kustaafu mchezo huo.
LeBron ndilo jina kubwa ambalo kwa muda mrefu liko juu kwenye thamani ya kitimu na kwake binafsi, kiasi cha kuifanya Lakers kutazamwa zaidi kote duniani hususan mechi za ligi zinazohusisha timu hiyo.
Kutokana na kubakiza misimu isiyozidi minne hadi mitano kabla ya kustaafu na pengine ikawa baada ya kumaliza mkataba wake miaka mitatu ijayo, inaelezwa mabosi wa timu hiyo wanamtazama Luka Doncic wa Dallas Mavericks kama mrithi sahihi wa LeBron miaka michache ijayo.
Hilo litatokana na hali ya Docic maarufu kama Magic katika timu ya Mavericks, lakini ubora na kile anachoweza kukifanya kwa sasa na misimu ijayo inampa nafasi kubwa ya kuwekewa lengo kuungana na Anthony Davis (AD) ambaye pia anaweza kutengenezewa ufalme baada ya LeBron.