Djokovic mikononi mwa Sinner, Alcaraz

Muktasari:
- Sinner alimtoa Djokovic kwenye michuano ya wazi ya Australia, huku Alcaraz akimchapa kwenye fainali ya michuano ya Ufaransa (Rolland Garros), ukiachana na iliyofuata ya Wimbledon nchini Uingereza ambayo yote Novak aliambulia patupu kabla ya kulipiza kisasi kwenye fainali ya Olimpiki nchini Ufaransa.
NDANI ya mwaka huu, staa wa tenisi kutoka Serbia, Novak Djokovic amekutana na wakati mgumu mbele ya vijana wawili hatari, Jannik Sinner na Carlos Alcaraz.
Sinner alimtoa Djokovic kwenye michuano ya wazi ya Australia, huku Alcaraz akimchapa kwenye fainali ya michuano ya Ufaransa (Rolland Garros), ukiachana na iliyofuata ya Wimbledon nchini Uingereza ambayo yote Novak aliambulia patupu kabla ya kulipiza kisasi kwenye fainali ya Olimpiki nchini Ufaransa.
Na sasa ni wakati wa kumalizia taji kubwa la tenisi lililobaki mwaka huu ambalo ni Marekani (US Open) lililoanza kufukuziwa wiki hii na linawakutanisha wababe hao watatu wanaolisaka kuongeza kwenye mataji ya mwaka huu.
Ili Djokovic aweke rekodi ya muda wote kwa kutwaa taji la 25, atakuwa na kazi mbele ya Sinner na Alcaraz, huku pembeni akiwepo Alexander Zverev wa Ujerumani ambaye hachezi mbali.