Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

De Gea anarudi

MANCHESTER, ENGLAND. BAADA ya mwendelezo mbaya wa kipa wa Manchester United, Andre Onana na hatari ya kukosekana kwake ifikapo mwakani, taarifa zimefichua benchi la ufundi la miamba hiyo limepanga kumrudisha kipa wa zamani wa timu hiyo, David de Gea katika dirisha lijalo la majira ya baridi kwa mkataba wa nusu msimu.

Mabosi wa Man United wanahofia kuwa na idadi ndogo ya makipa kwa sababu Onana anatarajiwa kujiunga na Timu ya Taifa ya Cameroon mwakani ambapo ataenda kuitumikia timu hiyo kwenye michuno ya AFCON.

Akiondoka itawalazimu kumtumia kipa namba mbili, Tom Heaton ambaye haaminiki sana kama anaweza kwenda kulinda vizuri lango lao.

Michuano ya Afcon inatarajiwa kuanza Januari 13 hadi Februari 11, jambo linaloonesha kwamba Onana aliyesajiliwa kwa Pauni 43.8 milioni huenda akakosa mechi nane kama timu yake itacheza hadi fainali.

Hivyo, macho na masikio kwa sasa yapo kwa De Gea ambaye iliachana naye katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu.

Kipa huyu raia wa Hispania ambaye kwa sasa ana umri wa miaka , 32, kabla ya kuondoka alikuwa amedumu kwenye viunga vya Old Trafford kwa takribani miaka 12 na sasa yupo huru.

De Gea aliondoka baada ya majadiliano ya muda mrefu ambapo Man United ilihitaji akubali kupunguza mshahara wake kutoka Pauni 375,000 hadi 200,000 ambapo alikubali lakini mwishoni dili hilo liliondolewa mezani na Mashetani Wekundu wakaingia sokoni kutafuta kipa mpya.

Hata hivyo, mbali ya kuachana naye maofisa wa Man United walimtaka kipa huyu kutofikia makubaliano ya kujiunga na timu yoyote hadi pale wao watakapofanikisha mchakato wa kumpata Onana.

Suala hili halionekana kuwa la heshima kwa De Gea ambaye alidumu kwenye kikosi hicho kwa muda mrefu na alikuwa amemaliza msimu akiwa na tuzo ya glovu ya dhahabu kwa kucheza mechi nyingi bila ya kuruhusu bao.

Man United ilimnunua Altay Bayindir kutoka Fenerbahce kwa Pauni 4.3 milioni katika dirisha lililopita lakini wakati Onana atakapokuwa kwenye majukumu ya kuiwakilisha Cameroon kwenye AFCON kipa pekee atakayebakia kwenye kikosi chao atakuwa ni Tom Heaton.

Tetesi za De Gea kurudi zilizidi kupamba moto baada ya hivi karibuni kapteni wa Man United, Bruno Fernandes kuonekana akiwa kwenye picha ya pamoja na kipa huyo na akieleza hisia zake kwamba hakuagwa vizuri kama mmoja ya makipa walioitumikia timu hiyo kwa muda mrefu.

Lakini hilo linaweza kutokea pia ikiwa atakubali kuichezea timu hiyo kwa muda mfupi, pia baadhi ya mashabiki wanaamini kutokana na kiwango cha Onana kulikuwa na ulazima wa De Gea kubakishwa.

Mara kadhaa baadhi ya timu zilitajwa kwamba zinahitaji kumsaini kipa huyo lakini nyingi zimeshindwa kufikia mwafaka wa kuipata saini yake.