Danki 5 za kibabe NBA 2024-25
Muktasari:
- Teknolojia hii mpya, inayojulikana kama ‘NBA Dunk Score’, inachambua na kutoa alama kwa kila danki kwa kutumia vigezo mbalimbali kama vile uwezo wa kimwili wa mchezaji, ustadi wa kiufundi, na ugumu wa dunki husika.
CALIFORNIA, MAREKANI: KATIKA msimu wa NBA wa 2024-25, teknolojia ya kisasa na matumizi ya sayansi ya data ya NBA yameleta mabadiliko makubwa jinsi inavyopimwa na kufuatilia dank za wachezaji.
Teknolojia hii mpya, inayojulikana kama ‘NBA Dunk Score’, inachambua na kutoa alama kwa kila danki kwa kutumia vigezo mbalimbali kama vile uwezo wa kimwili wa mchezaji, ustadi wa kiufundi, na ugumu wa dunki husika.
Alama hii ni matokeo ya uchambuzi wa kina unaojumuisha vipengele kama vile nguvu ya mchezaji, kiwango cha kuruka, ufanisi katika kukutana na upinzani wa mlinzi, na jinsi mchezaji anavyoshuka baada ya kufanya danki.
Kwa mara ya kwanza, NBA inatumia mfumo huu kuangalia na kutoa alama kwa kila danki katika wakati halisi, jambo ambalo limeongeza uwazi na usahihi katika kutathmini ufanisi wa wachezaji katika michezo.
Kupitia mfumo huu, inapatikana picha halisi ya ni nani wanaoongoza kwa danki bora na ya kibabe zaidi msimu huu, na tunapata nafasi ya kulinganisha ufanisi wa wachezaji katika nyanja hii muhimu ya mchezo wa mpira wa kikapu.
Hii ni orodha ya dunki tano za kibabe (Top 5 NBA Dunk Scores) kwa msimu huu wa 2024-25, huku tukiangalia alama za wachezaji na kile kinachowafanya kuwa bora zaidi katika kipengele hiki cha kuvutia cha mchezo wa NBA.
1. John Collins (Utah Jazz) -113.4
Anaongoza orodha ya danki bora za msimu huu baada ya kufanya danki kali dhidi ya Chicago Bulls Novemba 4, 2024. Katika mchezo huo, Collins alionyesha uwezo wake mkubwa wa kimwili na kiufundi kwa kuruka juu ya mlinzi kwa urefu wa inchi 33, na kutupa mpira kwenye kikapu ‘rim’ kwa kasi ya 27 mph. Danki hii ilikuwa na alama ya kubwa katika vipengele vya nguvu ‘Power’ (96) na namna ya ulindaji ‘Defensive Contest’ (94), ambazo zote zilikuwa juu ya alama ya 90. Kwa kufanya hivyo, Collins alijitofautisha na wachezaji wengine akiwa na jumla ya alama 113.4.
2. Jalen Green (Houston Rockets) -111.3
Alifanya danki kali dhidi ya Detroit Pistons Novemba 10, 2024. Green alionyesha umahiri wake wa kimwili na uwezo wa kuruka kwa ufanisi mkubwa. Alikuwa na urefu wa 40.2 inches katika kuruka na alionyesha nguvu ya ajabu kwa kupata Power subscore ya 99, ambayo ni moja ya alama za juu zaidi katika kipengele cha nguvu kwa danki za msimu huu.
3. Jaylen Brown (Boston Celtics) -109.6
Alifanya danki kali dhidi ya Chicago Bulls Novemba 29, 2024 na kufikisha alama ya 109.6. Danki hii ilikuwa na alama kubwa, ikiwa ni pamoja na Max Ball Height ya 10.9 feet, ambayo ni ishara ya ufanisi mkubwa wa kuruka. Brown alionyesha umahiri mkubwa katika sehemu ya Power subscore, akifanikisha alama ya 91 katika kipengele hiki na alama ya Jump subscore ya 86. Hii ina maana Brown alifanya danki yenye nguvu kubwa huku akiwa na ufanisi mzuri katika kuruka kwa urefu wa juu.
4. Brandon Miller (Charlotte Hornets) - 108.9
Alifanya danki la kuvutia katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Houston Rockets Oktoba 23, 2024. Alianza msimu kwa nguvu, akifanya danki kali kwa inchi 36.1 na akapiga alama ya 108.9. Alikuwa na alama nzuri za Jump subscore (91) na Power subscore (94), na kutupa mpira kwenye kikapu ‘rim’ kwa ufanisi mkubwa.
5. Keegan Murray (Sacramento Kings) -107.6
Alifanya danki kali dhidi ya Minnesota Timberwolves Novemba 27, 2024, na alifanikiwa kufikisha alama ya 107.6. Murray alionyesha uwezo wake mkubwa wa kimwili kwa kuruka kwa urefu wa 33.2 inches, akiwa na umbali wa 7.3 feet kutoka kwa kikapu ‘rim’.
Danki nyingine za kibabe
Hii ni orodha ya wachezaji ambao pia wamepata alama za juu katika danki zao:
Christian Braun -106.3
Bruno Fernando -105.2
Giannis Antetokounmpo -102.3
Jaden Hardy -101.7
Yves Missi -101.0