Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Curry, Ayesha wakaribisha NBA All-Star kitaa

Muktasari:

  • Pamoja na hayo yote, Jumapili hii kutakuwa na mchezo wa All-Star wa NBA utakaopigwa mbele ya watazamaji zaidi ya milioni. Lakini kabla ya hilo, familia ya Curry akiwa sambamba na mkewe Ayesha ilianzisha shughuli za kijamii, ikiwemo kuhamasisha jitihada za kusaidia shule za msingi na watoto ambao wanahitaji msaada.

 CALIFONIA, MAREKANI: KWA familia ya nyota wa  Golden State Warriors, Stephen Curry, wikendi hii tangu juzi, Ijumaa ni mwendo wa pati tu na kutoa michango yao kwa jamii. Unaambiwa watu walikuwa wakinywa, kula na kusaza.

Pamoja na hayo yote, Jumapili hii kutakuwa na mchezo wa All-Star wa NBA utakaopigwa mbele ya watazamaji zaidi ya milioni. Lakini kabla ya hilo, familia ya Curry akiwa sambamba na mkewe Ayesha ilianzisha shughuli za kijamii, ikiwemo kuhamasisha jitihada za kusaidia shule za msingi na watoto ambao wanahitaji msaada.

Wikendi yao ilianza Ijumaa, ambapo waliongoza shughuli ya huduma ya kijamii kwa kushirikiana na shirika lao la Eat. Learn. Play. Foundation. Ilikuwa ni siku ya ukarabati wa uwanja wa michezo katika shule moja ya msingi huko Oakland.

Shughuli hiyo ilihusisha kupanda mimea 800, kubeba na kusambaza udongo kwa wingi, na kuzungumza na watu 300 ambao walijitokeza kusaidia. Pamoja na hayo, familia ya Curry ilikabidhi viwanja vya michezo vilivyorekebishwa, na kuonyesha wazi msaada wao wa kudumu kwa shule na watoto walioko kwenye mazingira magumu.Hili ni miongoni mwa matukio muhimu kwa familia ya Curry, kwani ni sehemu ya ahadi yao ya kuwa mstari wa mbele kusaidia jamii inayowazunguka, na siyo tu katika michezo.

Ayesha Curry alisema, “Tunaipenda Oakland (ni mji wa nane kwa ukubwa California). Hapa ndio tulikulia, hapa ndio tulianzisha maisha yetu pamoja na Stephen, na hapa ndipo tulipopata mtoto wetu wa kwanza. Oakland inatufanya tujihisi tukiwa na nguvu. Hata kama hatuwezi kuishi hapa kila siku, tumekuwa na ahadi ya kudumu kwa jamii hii, na tunaendelea kujitolea kwa kila njia.”

Licha ya ukweli kwamba Stephen Curry sasa anachezea timu ya Golden State Warriors iliyopo San Francisco, familia ya Curry imeendelea kudumisha uhusiano wao na Oakland.

Stephen Curry alielezea, “Tuna timu nzuri inayotuunga mkono, ambayo inachukua mwelekeo wa ahadi yetu kwa Oakland na inatumia nguvu hiyo kuleta mabadiliko makubwa kwa jamii. Huu ni ukarabati wetu wa 17 wa viwanja vya michezo, na kila tukio ni muhimu kwetu. Hii ni furaha yetu kuona watoto, walimu, na wafanyakazi wa shule wakifurahi kwa kuona maono yetu yakiwa halisi.”

Kwa upande mwingine, Stephen na Ayesha wamekuwa na mafanikio makubwa katika kazi zao binafsi. Stephen ni mmoja wa wachezaji bora wa mpira wa kikapu wa wakati wote, na ameshinda mataji manne ya NBA. Ayesha, mbali na kuwa mke wa nyota huyo, pia ni mpishi maarufu na mjasiriamali mwenye migahawa maarufu. Lakini ingawa wanavutiwa na kazi zao, familia ya Curry inaweka umuhimu mkubwa zaidi kwa kazi za nje ya uwanja. Ni kazi hizi zinazohusiana na kutoa msaada kwa jamii, kwa kutoa elimu, chakula bora, na kuhamasisha watoto kupitia programu zao mbalimbali za kijamii.

Shirika lao la Eat. Learn. Play. Foundation, lililoanzishwa miaka mitano iliyopita, limejikita katika misingi ya lishe bora, mazoezi, na elimu. Hivi karibuni, wamekuwa na umakini maalum kwa kukuza ufanisi wa watoto katika ufahamu wa kusoma, na kutengeneza fursa za elimu kwa watoto wanaotoka kwenye familia zenye changamoto. Ayesha alielezea umuhimu wa kufundisha watoto na kuhakikisha wanapata elimu bora. “Hii itawawezesha watoto kufanikiwa, kumaliza shule, na kuwa na maisha bora zaidi baadaye,” alisema Ayesha Curry.

Hata hivyo, licha ya kuwa na shughuli nyingi na ratiba ngumu, familia ya Curry haijalalamika. Stephen Curry ambaye ameshakuwa mchezaji wa All-Star mara 11, anasema kuwa fursa ya kuwa mwenyeji wa shughuli kubwa kama hii ni muhimu, na pia ni njia nzuri ya kuelezea kile ambacho Eneo la Bay linahusisha.

“Kwa upande wangu, hii ni nafasi ya kuangazia kila jambo tulilofanya katika kipindi cha miaka 16 hapa Bay Area. Ni wakati wa kusherehekea kile ambacho tumepitia, na kwa kweli, kuwa mwenyeji wa All-Star ni jukumu kubwa, lakini ni furaha kubwa pia. Wikendi hii itakuwa na mchakamchaka, lakini nashukuru kwa kila fursa ya kuonyesha furaha yetu kwa Eneo la Bay,” alisema Stephen Curry.

Kwa familia ya Curry, wikiendi hii ni zaidi ya mchezo wa mpira wa kikapu ni kipindi cha kutafakari, kusherehekea mafanikio, na kurudisha kwa jamii inayowazunguka. Kila tukio, iwe kubwa au ndogo, inatoa nafasi ya kuonyesha upendo wao kwa Oakland, Eneo la Bay, na watoto wanaohitaji msaada ili kufikia ndoto zao.