Chelsea yaokota dodo

ENGLAND, LONDON. NICOLAS Jackson analinganisha Mauricio Pochettino na mkufunzi wa Aston Villa Unai Emery anapofurahia maisha huko Chelsea ambapo amejiunga hivi punde.
Chelsea wamefanya usajili wa hivi karibuni kwa ada ya pauni milioni 32 kumpata mshambuliaji Jakson akitokea Villarreal ambaye alionyesha kuvutiwa kwake na meneja Pochettino, akiangazia matokeo chanya ambayo Muargentina huyo amefanya tangu kuwasili kwake Stamford Bridge.
Jackson alimsifu meneja huyo wakiargentina kwa kuwa na msimamo kama kiongozi akifananisha kocha mpya wa Chelsea na kocha wake wa zamani, Emery, tangu alipokuwa Villarreal.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alionyesha ujuzi wake katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Brighton Jumapili, akifunga bao na kutoa pasi mbili za mabao huku akionesha kiwango kikubwa na kumpa imani meneja wake mpya .
Akizungumza na vyombo vya habari vya ndani ya klabu hiyo baada ya mchezo wa Brighton, alisema; "Mambo yanakwenda vizuri sana, nina furaha sana hivi sasa. Uendeshaji sio mbaya hata kidogo, ni sawa. Kuna mambo yanayofanana kati ya bosi Pochettino na Unai Emery, ambaye alinifundisha Villarreal."
Nicolas amekuwa na ndoto kubwa yakuwa mmoja kati ya nyota waliopitia klabuni hapo ambao wamepata mafanikio makubwa pamoja na heshima ’’ikiwa naweza kuwa na mafanikio kama Drogba, Demba Ba, na Eden Hazard, basi nitafurahi. Ni magwiji wa Chelsea. Ikiwa ninataka kuzingatiwa kama gwiji, lazima niwe bora zaidi kuliko wao."
Matamshi mazuri ya mshambuliaji huyo kuhusu kocha wake mpya Pochettino yanaonyesha mwanzo mzuri wa maisha yake ya soka Chelsea chini ya uongozi wa meneja huyo wa Argentina. Utayari wa mchezaji huyo kukumbatia mahitaji ya kimwili yaliyowekwa na Pochettino inaonyesha kujitolea kwake kuzoea mtindo wa uchezaji wa timu.
Jackson akitua vyema Chelsea na kujenga ukaribu na wachezaji wenzake, fowadi huyo chipukizi wa Senegal atatarajia kuendelea kufanya vizuri chini ya uelekezi wa kocha wake, akianza na mechi zao za kabla ya msimu mpya. Chelsea wana mechi zijazo za kirafiki dhidi ya Newcastle, Fulham, na Borussia Dortmund.