Chelsea yamvutia kasi Aubameyang

MATAJIRI wa London, Chelsea wameingia vitani kusaka saini ya mshambuliaji wa Barcelona, Pierre Emerick Aubameyang.

Aubameyang kwa sasa anatazamwa kama mrithi wa Romelu Lukaku ambaye ameondoka Stamford Bridge kwa kurejea zake Inter Milan.

Lukaku aliamua kurejea zake Inter Milan baada ya mambo kumwendea kombo chini ya Thomas Tuchel ambaye alikuwa akimweka benchi mshambuliaji huyo.

Tuchel anamtazama Aubameyang  kama mabadala sahihi wa mshambuliaji huyo kutokana na wawili hao kufanya kazi pamoja huko Ujeruman kwenye klabu ya Borussia Dortmund.

Inaweza kuwa rahisi kwa Aubameyanga kuondoka Barcelona na kurejea kwenye Ligi ya England kutokana na Barcelona kusajili Robert Lewandowski.

Kama ataendelea kusalia inamaana kuwa huenda Mgabon huyo akapoteza nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo hivyo Tuchel anataka kutumia mwanya huo.