Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamondi karudi Bara, yupo Singida BS mjipange!

Muktasari:

  • Uongozi wa Singida umemtangaza Gamondi kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho msimu ujao wa 2025/26 na kumbadilishia majukumu David Ouma.

KOCHA wa zamani wa Yanga, Miguel Gamondi amerudi rasmi katika Ligi Kuu Bara baada ya kutangazwa kuwa kocha mkuu wa Singida Black Stars.

Uongozi wa Singida umemtangaza Gamondi kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho msimu ujao wa 2025/26 na kumbadilishia majukumu David Ouma.

Gamondi amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuifundisha timu hiyo, hivyo wasaidizi wake  watakuwa Ouma na Moussa N'Daw ambaye ni igizo jipya.

Taarifa hizo zimetolewa na Msemaji wa timu hiyo, Hussein Masanza kwamba bodi ya Wakurugenzi imefanya mabadiliko hayo kujipanga na msimu ujao.

"Baada ya uwepo wa tetesi nyingi tumeona tuliweke jambo hilo sawa, Gamondi amesaini mkataba wa mwaka mmoja, Ouma amebadilishiwa majukumu atakuwa msaidizi," amesema.

Gamondi ana uzoefu na mpira wa miguu Tanzania, kwa mara ya kwanza alijiunga na Yanga msimu wa 2023/24 ambao alichukua ubingwa wa Ligi Kuu kisha akaondoka Novemba 15, mwaka jana, hivyo anatarajiwa kuwa msaada katika ligi ya ndani na Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Ouma ambaye amebadilishiwa majukumu msimu uliyoisha ameisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya nne katika Ligi Kuu Bara kwa pointi 57 na kucheza fainali za Kombe la Shirikisho (FA)  na kupoteza 2-0 kwa Yanga iliyotetea taji kwa msimu wa nne mfululizo.