Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cazorla, Arteta kuna kitu kinakuja

Muktasari:

  • Kiungo huyo Mhispaniola kwa sasa anacheza kwenye kikosi cha Real Oviedo ambacho kimepambana kupanda daraja na kucheza La Liga, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 23, ikitokea Segunda Division.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO fundi wa mpira, Santi Cazorla amefichua namna alivyojadiliana na kocha wa Arsenal, Mikel Arteta kwa ajili ya kurejea kwenye kikosi hicho cha Emirates, wakati huu akijiandaa kutundika daruga zake kwenye majira haya ya kiangazi huko Ulaya.

Kiungo huyo Mhispaniola kwa sasa anacheza kwenye kikosi cha Real Oviedo ambacho kimepambana kupanda daraja na kucheza La Liga, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 23, ikitokea Segunda Division.

Cazorla, 38, alirejea kwenye klabu yake hiyo ya utotoni mwaka jana na aliomba asilipwe mishahara. Oviedo kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya kucheza mechi ya mchujo ya kupanda daraja na mechi ya kwanza ilimalizika kwa sare ya bila mabao dhidi ya Eibar.

Cazorla hakucheza kwenye mechi hiyo ya kwanza. Kiungo huyo anayepiga miguu yote miwili kwa ubora uleule aliweka wazi kwamba atatundika daruga, lakini sasa amefungua milango ya kurejea Emirates, alikowahi kutamba wakati huo Arsenal ilipokuwa chini ya Arsene Wenger.

Cazorla aliichezea Arsenal kwa miaka sita na kuwa kipenzi cha mashabiki kwenye timu hiyo, huku Arteta alikuwa swahiba wake mkubwa walipotamba pamoja kwenye safu ya kiungo ya miamba hiyo.

Kocha Arteta alimfungulia milango Cazorla ya kwenda kujiunga na benchi la ufundi la timu hiyo, huku mwenyewe akiweka wazi kwamba yupo tayari kurudi kwenye klabu yake hiyo ya zamani.

“Nimekuwa na muunganiko wa kipekee kabisa na Arsenal,” alisema Cazorla na kuongeza. “Nicheza kwa miaka sita pale yenye mafanikio makubwa kabisa na nafahamu watu namna wanavyonipenda. Nilikuwa vizuri na Mikel Arteta, ambaye kwa sasa ni kocha. Tulikuwa na majadiliano ya kuhusu kurudi kwenye timu hiyo, lakini kwa sasa, nikiwa bado mchezaji wa Oviedo, akili na mawazo yapo kwenye kuisaidia timu hiyo kupanda daraja.”