Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bayern inamsaka Nkunku kimyakimya

Nkunku Pict

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa Stamford Bridge hafurahishwi na idadi ya mechi anazocheza kwenye Ligi Kuu England akianzia benchi mara nyingi chini ya kocha Enzo Maresca baada ya msimu wake wa kwanza kuwa nje ya uwanja muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi.

MUNICH, UJERUMANI: BAYERN Munich imeripotiwa kuwa tayari kufikia makubaliano na staa wa Chelsea, Christopher Nkunku ikihitaji saini yake kwenye dirisha hili la Januari.

Fowadi huyo wa Stamford Bridge hafurahishwi na idadi ya mechi anazocheza kwenye Ligi Kuu England akianzia benchi mara nyingi chini ya kocha Enzo Maresca baada ya msimu wake wa kwanza kuwa nje ya uwanja muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi.

Fowadi huyo Mfaransa amefunga mabao 13 msimu huu, ambapo mabao 11 amefunga kwenye mechi 10 za michuano ya makombe.

Bayern imefikia makubaliano ya mdomo na Nkunku na mpango wao ni kumpa mkataba mrefu mchezaji huyo endapo kama watakubaliana jambo na Chelsea.

Nkunku anavutiwa na mpango wa kwenda kujiunga na miamba hiyo ya Bundesliga kwenye dirisha hili la Januari, huku Bayern yenyewe ikimweka kwenye chaguo lao la kwanza katika wachezaji inaowahitaji.

Na sasa imeelezwa kinachoendelea ni kwamba Bayern ilikuwa kwenye mazungumzo na kinda Mathys Tel, 19 ili atumike kwenye dili la kubadilishana na Nkunku. Lakini, kama Tel atang’ang’ania kubaki Allianz Arena, Bayern haitafuta mpango wake wa kumsajili Nkunku.

Chelsea ilionyesha kuvutiwa na kinda huyo Mfaransa kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana, hivyo itavutiwa na mpango wa Bayern endapo kama utamhusisha Tel, ambaye alisaini mkataba mpya miezi 12 iliyopita, ambapo utamfanya abaki Allianz Arena hadi 2029.

Kinda huyo wa zamani wa Rennes amecheza mechi saba tu chini ya kocha Vincent Kompany msimu huu na kinachoelezwa ni kwamba mchezaji alimwambia kocha wake mapema mwezi huu kwamba atakuwa mwenye furaha kama atakuja kupata mafanikio makubwa akiwa na kikosi cha Bayern.

Nkunku kwa upande wake alizungumza na kocha Maresca juu ya hatima yake kwenye kikosi cha Chelsea, ambacho alijiunga nacho mwaka 2023 akitokea RB Leipzig kwa ada ya Pauni 52 milioni.