Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AJ amkataa Tyson kwa Usky

Muktasari:

  • Joshua ‘AJ’ anayetarajia kuzichapa na Daniel Dubois Septemba 21 mwaka huu, ameshindwa kuficha hisia zake za anavyotarajia kwenye pambano baina ya Tyson na Usyk mwezi Desemba na amemkataa kabisa Tyson kulipiza kisasi kwa Usyk.

WAKATI akiwa na takriban mwezi mmoja kabla ya kupanda ulingoni mwezi ujao, bondia Anthony Joshua wa Uingereza, kwa mara nyingine amezungumzia pambano baina ya ndugu yake Tyson Fury dhidi ya Oleksandr Usyk wa Ukraine.


Joshua ‘AJ’ anayetarajia kuzichapa na Daniel Dubois Septemba 21 mwaka huu, ameshindwa kuficha hisia zake za anavyotarajia kwenye pambano baina ya Tyson na Usyk mwezi Desemba na amemkataa kabisa Tyson kulipiza kisasi kwa Usyk.


Hii ni licha ya Tyson kutoka nchi moja na AJ (England) na  aliwahi kuzichapa na Usyk na mara zote mbili alishindwa kwa pointi za majaji, pengine ingekuwa sababu ya kutompa nafasi Usyk lakini amesisitiza ndiye ana nafasi kubwa ya kushinda pambano la marudiano dhidi ya Fury.


Mbali na kumpa nafasi Usyk kwenye pambano la marudiano, AJ pia amekiri kuhitaji sana pambano dhidi ya Tyson mwakani 2025 na itapendeza kama wote watashinda mapambano yao yajayo akianza yeye kuzichapa na Dubois kabla ya Fury kumalizana na Usyk Desemba 21.


Bondia mwingine aliyeonyesha wasiwasi Kwa Fury dhidi ya Usyk ni Otto Wallin ambaye amekiri Tyson atatakiwa kufanya kazi ya ziada ili alipe kisasi vinginevo atakuwa kwenye wakati mgumu sana kumpiga Usyk kwenye pambano hilo la marudiano.