Ni Lebron vs Ant Man, Tatum vs Brunsion NBA

Muktasari:
- Supastaa LeBron James wa Los Angeles Lakers ndiye aliyeibuka MVP wa Olimpiki na atarejea uwanjani kwenye ligi ya NBA siku ya kwanza ya ufunguzi wa ligi hiyo, kukipiga dhidi ya Minnesota Timberwolves ya Anthony Edwards ‘Ant Man’ itakayotanguliwa na mchezo wa Ukanda wa Mashariki.
HATIMAYE Oktoba 22 ndio tarehe rasmi ya kuanza kwa ile Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) baada ya kumalizana na shughuli ya Olimpiki iliyoshuhudia taifa hilo, likibeba tena taji hilo kwa mara ya tano mfululizo.
Supastaa LeBron James wa Los Angeles Lakers ndiye aliyeibuka MVP wa Olimpiki na atarejea uwanjani kwenye ligi ya NBA siku ya kwanza ya ufunguzi wa ligi hiyo, kukipiga dhidi ya Minnesota Timberwolves ya Anthony Edwards ‘Ant Man’ itakayotanguliwa na mchezo wa Ukanda wa Mashariki.
Boston Celtics ambao ndio mabingwa mtetezi siku hiyo itacheza dhidi ya New York Knicks katika uwanja wa TD Garden Arena uliopo Ukanda wa Mashariki na ndipo watakabidhiwa na pete zao za ubingwa wa NBA waliochukua msimu uliopita.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali kutokana na ubora mpya wa Knicks ambayo imempa unahodha Jalen Brunson tangu mara ya mwisho ilipokua mwaka 2018 na Knicks inatajwa kuwa tishio kwa Celtics msimu ujao.