De Jong kumfuata Ten Hag OT

Friday May 13 2022
Jong PIC

MANCHESTER, ENGLAND. MANCHESTER United imeripotiwa inakaribia kunasa saini ya kiungo wa Barcelona, Frenkie De Jong pindi na atajiunga nao baada ya kumalizana na mabosi wake wa sasa mwisho wa msimu.

Kabla ya kujiunga na Barca 2019, De Jong alikuwa Ajax iliyokuwa chini ya Erik Ten Hag aliyeteuliwa kuwa kocha mkuu wa Manchester United mwezi uliyopita.

Licha ya De Jong kuonyesha mchango mkubwa kikosi cha kwanza Barcelona kinachonolewa na Xavi, lakini kiungo huyo anataka kuondoka msimu utakapoisha kutafuta chngamoto sehemu nyingine.

Man United inasaka kiungo sahihi atakayecheza sambamba na Bruno Fernandes msimu ujao na hadi sasa bado hakijaeleweka endapo Paul Pogba atabaki kukipiga Old Trafford.

Taarifa zinadai, Barcelona ina mpango wa kuuza baadhi ya mastaa wake na kununua wengine kutokana na sababu za kiuchumi, huku De Jong akiwa sehemu ya mpango huo wa kupigwa bei.

De Jong amecheza mechi 29 za La Liga akiwa na Barca na 45 msimu huu na amecheza jumla ya mechi 138 huku mafanikio yake yakianza kuonekana akiwa na Ajax.

Advertisement

Katika msimu wake wa mwishio Ajax, alitoa mchango kwa kocha wake aliyemnoa Ten Hag, Ajax ikitinga nusu fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya kabla ya kuangukia pua kwa Tottenham.

Pia alibeba taji la Ligi Kuu ukiwa na klabu hiyo kabla ya kutua Barca na kubeba taji la Copa del Rey.

Advertisement