Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yusuph Athuman arudi bongo

Yusuph Pict

Muktasari:

  • Athuman alijiunga na timu hiyo Aprili mwaka huu akitokea Tanzania Prisons, aliyokuwa anaitumikia kwa mkopo akitokea Fountain Gate, ambayo hakuwahi kuichezea mchezo hata mmoja.

MSHAMBULIAJI Yusuph Athuman aliyekuwa anakipiga Yangon United inayoshiriki Ligi Kuu ya Myanmar amesema amerejea nchini baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo nchini humo.

Athuman alijiunga na timu hiyo Aprili mwaka huu akitokea Tanzania Prisons, aliyokuwa anaitumikia kwa mkopo akitokea Fountain Gate, ambayo hakuwahi kuichezea mchezo hata mmoja.

Akizungumza na Mwanaspoti, Athuman alisema amerejea nchini lakini hajaonekana Fountain Gate kutokana na kufungiwa kusajili wachezaji na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Aliongeza kama mambo yatakuwa sawa na Fountain itafunguliwa kusajili wachezaji, basi atarejea, ikishindikana itabidi atafute timu nyingine.

“Nafikiri nitarudi Fountain kwa sababu wao ndio waajiri wangu, lakini itategemea na mazingira ya klabu. Kama itafunguliwa itakuwa vyema, isipotokea basi usishangae kuniona kwenye klabu nyingine.”

“Kwa muda mchache niliocheza nimeongeza kitu kwenye soka langu, lakini inanifanya niendelee kujiimarisha zaidi kutokana na ushindani niliouona Asia.”

Nyota huyo wa zamani wa Yanga alitua Yangon United kwa miezi miwili tu, akitambulishwa Aprili mwaka huu lakini hakucheza mchezo hata mmoja.