Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga ishindwe yenyewe!

YENYEWE Pict

KATIKA maboresho ya kikosi cha Yanga kwa ajuili ya msimu ujao wa 2025-2026, Yanga imepanga kufanya usajili wa kuziba maeneo machache ikiwemo eneo la beki wa kati.


Kwa sasa eneo hilo lina vitasa wa maana, Ibrahim Bacca, Dickson Job na nahodha, Bakar Mwamnyeto, lakini benchi la ufundi limepiga hesabu ya kuongeza kifaa kingine kipya ili kujiandaa na msimu ujao ikiendelea kushiriki LIgi ya Mabingwa Afrika na kusaka mataji ya Ligi na Kombe la FA.


Katrika mchakato huo wa kusaka bveki wa kati, mwanzoni Mwanaspoti liliripoti Mkongomani, Henock Inonga aliyewahi kuitumikia Simba anatajwa kutakiwa na Yanga.

Sasa habari nzuri kwa Yanga ni kilichobaki sasa ishindwe yenyewe kwani taarifa kutoka Morocco zinabainisha kocha mkuu wa AS FAR Rabat, Alex Santos haoni nafasi ya kumtumia Inonga msimu ujao.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kocha Santos haoni nafasi ya Inonga kikosini kwake kwa msimu ujao, hivyo amemtoa kwenye mipango yake.

Habari kutoka Yanga, zinasema tayari mabosi wa klabu hiyo wameanzisha mazungumzo na FAR Rabat ili kuona kama kuna uwezekano wa kuipata saini ya beki huyo, kwa vile bado ana mkataba wa mwsaka mmoja na kikosi hicho kilichomsajili mwanzoni mwa msimu huu kutoka Simba.

Beki huyo wa kimataifa wa DR Congo, anapigiwa hesabu za kutua Yanga kuongeza nguvu eneo la ulinzi la kati linaloongozwa na Dickson Job na Ibrahim Hamad ‘Bacca’.

“Yanga ina uhitaji mkubwa wa kusajili mchezaji wa eneo hilo. Ila kuhusu nani anakuja ni mapema kuzungumza kwa sasa, lakini mchakato unaendelea na majina ya wachezaji wanaotazamwa kwa ajili ya kuongeza nguvu eneo hilo yapo mezani na tayari yameanza kufanyiwa mchakato na jina la Inonga ni miongoni mwao,” alisema mtoa taarifa huyo ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi.

Chanzo hicho kilisema mchakato wa kutafutwa kwa beki huyo ulianza baada ya kuachana na Gift Fred kutoka Uganda na tangu hapo Yanga wamekuwa na wakati mgumu kupata mchezaji ambaye ataweza kuendana na ushindani uliopo hasa kwenye eneo hilo.

Inonga amekuwa beki tegemeo kwa sasa wa kikosi cha AS FAR Rabat, kilichoondolewa katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa na Pyramids ya Misri kwa jumla ya mabao 4-3 baada ya awali kufungwa 4-1 ugenini na kuja kushinda nyumbani mabao 2-0.

“Kwa sasa mikakati mikubwa ambayo inafanywa ni kuhakikisha taji la Ligi Kuu Bara linabaki Jangwani kwa msimu wa nne mfululizo huku mambo mengine ya usajili yakifanyiwa kazi kimya kimya kabla ya msimu mpya kuanza kwani mikakati ni kuhakikisha timu ikianza kambi msimu mpya kila mchezaji ambaye ataitumikia Yanga atakuwa anafahamika,” alisema mtoa taarifa huyo.

Kabla ya kutua Simba mwanzoni mwa 2021/22, Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kumtaka Inonga na mwenyewe aliithibitishia Mwanaspoti katika mahojiano akisema mazungumzo na Wananchi yalifika mbali kwa kukubaliana kila kitu.

Alisema akiwa katika hatua za mwisho kufanya uamuzi Yanga, alipokea simu kutoka kwa kiongozi mwingine wa juu wa Simba ambaye naye alimueleza kuhitajika katika timu hiyo huku wakimwekea masilahi makubwa mezani kuliko yale ya Yanga.

Inonga alisema Yanga ilifanya kila kitu kwa ajili yake na ilikuwa inamsubiri nchini ili kuja kumalizana nayo kwa ajili ya kuitumikia kwa mkataba wa miaka miwili.

“Dah! Nadhani ilikuwa imepangwa tu nije kucheza Simba, kwani nilifika mpaka uwanja wa ndege wa Kinshasa ili nije Tanzania, lakini hilo lilishindikana na nilibadili uamuzi na kuja siku nyingine kwa ajili ya Simba,” alinukuliwa Inonga katika mahojiano hayo.