Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanaume, wanawake KIUT zabeba ubingwa wavu Dar

WAVU Pict

Muktasari:

  • Kwa wanawake KIUT ilifanikiwa kuifumua TPA kwa seti 3-1 katika mchezo wa fainali ya ligi hiyo na bingwa huyo aliondika na kitita cha Sh1 milioni, medali na kombe, huku TPA ikishika nafasi ya pili na kupata zawadi ya Sh500,000, medali na kombe ilhali Jeshi Stars ikipata Sh250,000 na medali.

TIMU za wanawake na wanaume za KIUT zimetawazwa kuwa mabingwa wa Ligi ya Mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es Salaam maarufu kama Serie A.

Kwa wanawake KIUT ilifanikiwa kuifumua TPA kwa seti 3-1 katika mchezo wa fainali ya ligi hiyo na bingwa huyo aliondika na kitita cha Sh1 milioni, medali na kombe, huku TPA ikishika nafasi ya pili na kupata zawadi ya Sh500,000, medali na kombe ilhali Jeshi Stars ikipata Sh250,000 na medali.

Kwa upande wa wanaume KIUT iliibuka na ushindi wa seti 3-0 dhidi ya High Voltage katika hatua ya fainali, hivyo bingwa kuondoka na kitita cha Sh1 milioni, kombe na medali, huku High Voltage imeshika nafasi ya pili alipata Sh500,000, medali na kombe na TPA ilimalizia nafasi ya tatu akipata Sh250,000 medali na kombe.

Mabingwa wa Serie B ni IP Sports ambao wataugana na TPDC pamoja na Nyika upande wa wanaume na kwa upande wa wanawake bingwa ni Chui, TPDC na Wazo waliopata nafasi ya kupanda kucheza Seria A katika ligi ya mkoa ya mwaka ujao.

Akizungumza baada ya ligi hiyo kumalizika, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TVF), Magoti Mtani amesema matarajio ni kuwaona mabingwa wa michuano hiyo wakionyesha ushindani kwenye michuano ya Ligi ya Taifa (TVNL) itakayofanyika mwezi ujao.

Ameutaka uongozi wa mkoa huo kuiendeleza ligi hiyo, huku akimwaga pongezi kwa mamemeja ambao wamekuwa chachu ya kuleta timu uwanjani kwa kutumia gharama zao kuwa wanatambua mchango huo.

"Nawashukuru wadhamini waliojitokeza kusaidia na kuendelea nawaomba wengine waje kwa wingi kusaidia ligi ya mwakani," amesema Mtani.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es Salaam (DAREVA), Fredy Mshangama amesema wamefanikiwa kwa asilimia 90 katika ligi ya mwaka huu kutokana na kushirikisha timu nyingi na kwamba, mafanikio hayo ni pamoja na ongezeko la timu ambayo ni chachu ya kuvutia wawekezaji kwani hamasa na ushindani vimekua kwa kiasi kikubwa.

Kocha wa KIUT, Said Alhaji Issa amesema kufanya mazoezi kwa bidii na kufuata maelekezo ndio siri ya ushindi wao kwa timu zote mbili kutwaa mwaka huu.

"Kwa wanaume mchezo ulikuwa mgumu kwani mpinzani wetu High Voltage walitufunga mzunguko wa kwanza 3-1 na mzunguko wa pili 3-1, hivyo tulirudi kukaa chini kutafakari vitu gani tufanye ili tushinde na tumeweza kufanikiwa," amesema.