Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida Black Stars yaanza na mashine hii

SINGIDA Pict

Muktasari:

  • Singida ambayo imeshajikatia tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao sawa na Azam FC imeanza kufanyia maboresho kikosi hicho.

UNAMKUMBUKA kiungo mshambuliaji Raouf Bao ambaye alionyesha kiwango bora katika mashindano ya Mapinduzi Cup 2025 yaliyofanyika Zanzibar akiwa na kikosi cha timu ya taifa Burkina Faso? Sasa inaelezwa nyota huyo wa AS Sonabel ya Ouagadougou yupo katika mazungumzo ya kina na klabu ya Singida Black Stars, ili kutua kwa msimu ujao wa mashindano.

Singida ambayo imeshajikatia tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao sawa na Azam FC imeanza kufanyia maboresho kikosi hicho.

Inaelezwa kila kitu kimekwenda sawa kwenye mazungumzo ya pande zote mbili na muda wowote kuanzia sasa atasaini mkataba wa miaka mitatu.

Hata hivyo, inaelezwa ujio wa kiungo huyo ambaye pia ana uwezo wa kucheza winga zote mbili utakuwa mbadala wa Authur Bada anayehusishwa na Yanga.

"Makubaliano yote yamefikiwa na mkataba wa miaka mitatu unatarajiwa kusainiwa muda wowote kuanzia sasa, tulianza kumfuatilia wakati ule alipokuja Zanzibar kwenye mashindano ya Mapinduzi lakini alikuwa bado hajanaliza mkataba na klabu yake," kilisema chanzo na kuongeza;

"Ni mchezaji mzuri ambaye aliwavutia viongozi na kubwa zaidi ni umri wake bado mdogo kwa hiyo kilichosalia ni kusaini mkataba na timu tu kwani amekubali ofa aliyowekea na pia anatamani kucheza Tanzania."

Mwanaspoti lilipomtafuta Afisa Habari wa timu hiyo, Hussein Masanza kuthibitisha dili hilo simu yake haikupatikana.

Kabla ya kujiunga na AS Sonabel, kiungo huyo aliitumikia RC Kadiogo pia ya Burkina Faso na msimu 2022/23 alicheza mechi nne za Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kuondolewa hatua za awali na kuangukia Kombe la Shirikisho ambako pia alicheza mechi mbili za makundi.