Moussa Camara kipa bora 2024/25

Muktasari:
- Camara ameibuka kipa bora baada ya mshindani wake mkubwa, Djigui Diarra wa Yanga kukosekana katika mechi dhidi ya Dodoma Jiji iliyopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar, kufuatia kucheza nyota wenzake, Aboutwalib Mshery.
Nyota wa Simba, Moussa Camara ameibuka kipa bora wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2024-2025, baada ya kufikisha 'Clean Sheets' 19, ikiwa ni msimu wake wa kwanza hapa nchini tangu ajiunge na kikosi hicho akitokea Horoya AC ya kwao Guinea.
Camara ameibuka kipa bora baada ya mshindani wake mkubwa, Djigui Diarra wa Yanga kukosekana katika mechi dhidi ya Dodoma Jiji iliyopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar, kufuatia kucheza nyota wenzake, Aboutwalib Mshery.
Diarra amekosa tuzo hiyo kwa msimu wa pili mfululizo baada ya msimu uliopita wa 2023-2024, kumaliza na 'Clean Sheets' 14, akizidiwa ujanja na aliyekuwa kipa wa Coastal Union, Mkongomani Ley Matampi aliyeibuka kidedea kwa kufikisha 15.
Matampi aliyejiunga na Coastal Union Aug 31, 2023, akitokea Jeunesse Sportive Groupe Bazano ya kwao DR Congo, aliondoka Desemba 10, 2024, kwa makubaliano ya pande mbili ya kusitisha mkataba wake na kikosi hicho, uliokuwa unaisha msimu huu.