Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yawageukia wazee

Muktasari:

  • Kituo hicho cha Petra Elderly kinajenga kituo cha kisasa cha kuwatunza, kuwahudumia na kunufaika na mafunzo na busara za wazee.

UONGOZI wa klabu ya Yanga ikishirikiana na wadhamini wao GSM imekabidhi rasmi kiasi cha Sh 200 milioni sambamba na mifuko ya saruji yenye ujazo wa tani 100 katika ujenzi wa makazi ya kisasa ya kuwalea wazee wenye uhitaji.

Kituo hicho cha Petra Elderly kinajenga kituo cha kisasa cha kuwatunza, kuwahudumia na kunufaika na mafunzo na busara za wazee.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said alisema saruji hiyo na fedjha hizo ni kutumiza ahadi yao waliyoitoa Oktoba 27 kwenye hafla maalum ya kuchangia fedha za ujenzi wa kituo hicho.

Hersi alisema Yanga inatambua mchango wa wazee kwenye jamii ambapo klabu hiyo kongwe ikishirikiana na Taasisi ya GSM wamefanikisha ahadi yao hiyo ambayo waliitoa wakati wa uchangiaji hafla iliyoongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete.

"Yanga tunafanya kazi kwa karibu na wadhamini wetu, ukiacha mashirikiano ya kimsingi ya kimkataba na tulipoletewa jambo hili linalohusu jami hasa wazee tuliona umuhimu wa kuwa sehemu ya watakaofanikisha ujenzi wa kituo hicho," alisema Hersi.

"Siku ya hafla ile tulitoa ahadi ya kutoa mifuko ya saruji tani 100 lakini pia wadhamini wetu GSM kupitia taasisi yao nao walitoa ahadi ya kutoa sh 200 milioni ambavyo vyote hivi tutavikabidhi leo hapa."