Yanga yatua kibabe Mwanza, Kaze aishtukia Mwadui

Yanga tayari imewasili viunga vya Kanda ya Ziwa tayari kuwavaa Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa Jumamosi Desemba 12 mjini Shinyanga.


Kikosi hicho chini ya benchi lake la ufundi, likiongozwa na Kocha Mkuu, Cedrick Kaze, na viongozi wa juu, ikiwa ni Makamu Mwenyekiti, Frederick Mwakalebela na Mtendaji Mkuu Senzo Mazingisa wamewasili jijini hapa kwa mapokezi makubwa.

Mashabiki wa timu hiyo waliwasili Uwanja wa Ndege wa Mwanza saa saba mchana na kuisubiri timu hadi ilipotua saa 10:05 jioni na kuwasindikiza kwa shangwe.

Kwa sasa Yanga ndio timu pekee katika Ligi Kuu ambao hawajapoteza mechi yoyote katika michezo 14 waliyocheza na kukaa kileleni kwa alama 34, huku Mwadui wakiwa nafasi ya 17.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Cedrick Kaze amesema anafahamu kilichowakuta watani zao Simba huko mjini Shinyanga msimu uliopita, hivyo wamejipanga kuendeleza ushindi katika Ligi Kuu.

Katika msimu uliopita, Simba ikiwa chini ya Kocha, Patrick Aussems ilijikuta ikilala dhidi ya Mwadui FC bao 1-0 baada ya kucheza mechi saba bila kupoteza mchezo wowote katika uwanja wa CCM Kambarage mjini humo.


“Mwaka jana Simba mechi ya kwanza walipotezea Shinyanga, najua ni mechi haitakuwa rahisi hatutaangalia msimamo. Tumejiandaa na wachezaji wako vizuri,” amesema Kaze

Akizungumza jijini Mwanza, Kaze amesema anafahamu watani zao waliwahi kutibuliwa rekodi yao, hivyo amewaandaa vyema nyota wake kuhyanga 2 pic

akikisha wanapata pointi tatu.

Ameongeza kuwa anaelewa wanaenda kukutana na timu ambayo haina matokeo mazuri, ambapo kawaida timu za hivyo huwa zinakamia

“Tutahakikisha kila mechi tunachukulia kwa umakini mkubwa,” amesema Kaze

 NA Saddam Sadick