Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yatua Arabuni

YANGA Pict

MABOSI wa kikosi cha Yanga wajanja sana, kwani wakati timu hiyo ikijiandaa na mechi mbili z kufungia msimu za Ligi Kuu Bara na moja ya Kombe la Shirikisho (FA), lakini wenyewe wapo bize kuhakikisha wanaanza kusuka skwadi mpya kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano.


Katika kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa, tayari mabosi hao wameibuka Arabuni wakisaka beki wa kati ya kuwaongezea nguvu mabeki waliopo sasa akiwamo nahodha msaidizi, Dickson Job na Ibrahim Bacca wanaonza kikosi cha kwanza wakiwa sambamba na nahodha mkuu, Bakari Mwamnyeto.


Inaelezwa kuwa, mabosi hao wapo sokoni kusaka beki mpya na tayari wamerudha karata kwa kitasa wa Al Hilal ya Sudan, Mohamed Ahmed Saeed.

Beki huyo anayekipiga chini ya kocha Florent Ibenge, bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo, huku akiwa ni miongoni mwa wachezaji wanaochezea kikosi cha kwanza.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zililiambia Mwanaspoti ni kweli klabu hiyo imevutiwa na beki huyo kwani kati ya maeneo ya kuongeza nguvu msimu ujao na hilo lipo. “Tunahitaji kuboresha eneo la beki wa kati, japo Job na Bacca bado wapo, ila nguvu inatakiwa iongezeke ili waweze wapate changamoto. Beki huyu tulikutana naye mara mbili msimu uliopita na alionyesha kiwango kikubwa kwa hiyo tuko kwenye majadiliano nao kuona jinsi gani tutaweza kumpata,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Kama tukifanikiwa kumpata itakuwa jambo zuri ingawa ugumu upo kwenye mkataba alionao kwa hiyo tutaangalia uwezekano wa yeye kuvunja au sisi kumnunua.”

Ikumbukwe kuwa, kikosi hicho cha Al Hilal hakichezi Ligi ya Sudan kutokana na suala la usalama nchini humo na kwa sasa ipo Mauritania ilipotwaa taji la ligi ya nchi hiyo.

Safu ya ulinzi Yanga msimu huu inayoongozwa na wazawa hao wakisaidiana na Bakar Mwamnyeto, ikiwa imeruhusu mabao 10 tu ikiwa iliyofungwa machache zaidi katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikifuatiwa na Simba iliyoruhusu 11.

Mbali na beki huyo, Yanga imekuwa pia ikuhusishwa kusaka beki wa kulia akitakwa Ibrahima Keita anayekipiga TP Mazembe, opia kiungo mkabaji wa Gor Mahia, Enock Morrison na inaelezwa inamtolea macho winga wa Al Hilal, Jean Claude Girumugisha na inafanya mazungumza na straika kutoka Ivory Coast ambaye hata hivyo jina lake halijatajwa na inaelezwa kuna fagio litapita Jangwani.

Inaelezwa mabosi wa Yanga wanataka kufyeka baadhi ya wachezaji na kukisuka kikosi upya kwa ajili ya kuleta ufanisi chini ya kocha mpya anayesakwa kuchukua nafasi ya Miloud Hamdi baada ya kukerwa na timu hiyo kushindwa kuvuka makundi ya Ligi ya Mabingwa ikiwa ni msimu mmoja tangu icheze robo fainali ya michuano hiyo, lakini ikitokea kucheza fainali ya Shirikisho Afrika 2022-2023.