Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yacouba aamua kukimbilia FIFA

YACOUBA Pict

Muktasari:

  • Yacouba ambaye alisaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Tabora msimu huu, alipata majeraha katikati ya msimu jambo lililomfanya kukosa mechi nyingi.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga anayekipiga kwa sasa Tabora United, Yacouba Songne amesema amepeleka malalamiko Fifa, baada ya kutolipwa mshahara wa miezi minne na kutomaliziwa ada ya usajili.

Yacouba ambaye alisaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Tabora msimu huu, alipata majeraha katikati ya msimu jambo lililomfanya kukosa mechi nyingi.

Akizungumza na Mwanaspoti, nyota huyo alisema mkataba upo ukingoni Tabora United, lakini bado hajapewa malipo yake na pia hakumaliziwa kiasi cha ada ya usajili.

“Nimeipeleka Tabora United Fifa kwa kushindwa kunilipa stahiki zangu, lakini pia sehemu kubwa ya matibabu yangu nje nalipa mwe-nyewe badala ya timu,” alisema Yacouba.

Ukiachana na msharaha ambao sijaupata kwa takribani miezi minne, lakini pia hata ada yangu ya usajili sijamaliziwa mpaka sasa.”

Mshambuliaji huyo alicheza mchezo wa mwisho dhidi ya KMC Novemba 29 katika Uwanja wa KMC Complex, ambapo walitoka na ushindi wa mabao 2-0.

Hii sio mara ya kwanza kwake kumaliza msimu akiwa nje, jambo lililowahi kutokea hata alipokuwa Yanga baada ya kupata majeraha ya goti tena na kukosa msimu mzima.

Ndani ya mechi 14 alizocheza Yacouba akiwa Tabora alifunga mabao manne, huku kikosi kikiweka rekodi ya kushika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kikicheza michezo 28.

Mabosi wa Tabora United hawakupatikana jana kuzungumzia madai ya Yacouba.