Yanga yaanza na mabadiliko watatu

Wednesday June 22 2022
Kikosi PIC
By Thobias Sebastian

Mabingwa wa Ligi Kuu Bara Yanga itakuwa na mchezo wa mzunguko wa 27, dhidi ya Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa leo majira ya 12:30.

Katika mechi hiyo kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi amefanya mabadiliko ya kikosi cha kwanza kwa kuwaweka nyota watatu benchi na kuwaanzisha wengine.

Wachezaji wa kikosi cha kwanza walioanzia benchi wapo, Djuma Shabani, Djigui Diarra na Yanick Bangala.

Nafasi zao walichukua Aboutwalib Mshery alianza baada ya Diarra, David Bryson alichukua nafasi ya Djuma wakati Ibrahim Bacca alianza kwa Bangala.

Kikosi cha Yanga kilianza na kipa, Mshery, mabeki wanne walikuwa Kibwana Shomary, Bryson na Ibrahim Bacca.

Viungo wa kati walikuwa Khalid Aucho, Salum Abubakar na Feisal Salumu wakati mawinga walikuwa Chico Ushindi na Ducapel Moloko.

Advertisement

Kinara wa mabao kwenye kikosi cha Yanga, Fiston Mayele alianza kwenye kikosi cha kwanza kama kawaida ilivyokuwa kwenye michezo mingi ya ligi msimu huu.

Yanga ilianza na mabadiliko hayo kutokana na baadhi ya wachezaji kucheza mfululizo huku wengine wakipumzishwa kwa ajili ya kombe la Shirikisho ASFC.

Benchi la akiba walikuwepo, Diarra, Bangala, Djuma , Yassin Mustapha, Deus Kaseke, Dickson Ambundo, Denis Nkane, Yusuph Athumani na Heritier Makambo.

Advertisement