Yanga noma, yaifunika Simba

Muktasari:

HAWAJABEBA ubingwa misimu minne mfululizo lakini kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ndiyo timu iliyoingiza watazamaji wengi.

HAWAJABEBA ubingwa misimu minne mfululizo lakini kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ndiyo timu iliyoingiza watazamaji wengi.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imetoa orodha ya timu 20 namna zilivyovuna mashabiki wengi waliojitokeza kutazama mechi za ligi hiyo kwa msimu wa 2020-21, huku timu 18 zikiwa za Ligi Kuu na mbili za daraja la kwanza.

Licha ya Yanga kumaliza nafasi ya pili huku watani zao Simba wakilitwaa taji la ligi hiyo, lakini wamepigwa bao kwa idadi kubwa ya watazamaji walioshuhudia michezo yao katika michezo 34 iliyopigwa ndani ya msimu.

Katika takwimu hizo Yanga iliingiza watazamaji 141,681 ambao waliingiza Sh986, 826,000 huku Simba wakishika nafasi ya pili baada ya michezo yao kuingiza watazamaji 138,518 ambao walipelekea kupatikana Sh929, 705,000.

JKT Tanzania iliingiza Sh148, 145,000 baada ya michezo yao kushuhudiwa na watazamaji 25,062 huku Dodoma Jiji iyoingiza watazamaji 27,455 walioingiza Sh 139,300,000.

Licha ya kushuka daraja msimu uliopita Ihefu haikuwa nyuma iliingiza Sh138,650,000 baada ya kupata watazamaji 19,903 huku Mtibwa Sugar ikiingiza  Sh120,037,000 kwa watazamaji 16,240 nao Mwadui FC walingiza mashabiki 22,232 ikiingiza Sh117,868,000.

Kwa taarifa zaidi soma gazeti la Mwanaspoti kesho Alhamisi Septemba 23, 2021