Yanga Arusha yatoa msaada kwa watoto yatima

Thursday August 04 2022
arusha pic
By Kennedy Lucas

ARUSHA. Wanachama na mashabiki wa Yanga tawi la Arusha Bus Terminal wameendelea kuadhimisha wiki ya Wananchi kwa kushiriki shughuli za kijamii.

Ikumbukwe Yanga inatarajia kuadhimisha kilele cha siku ya Mwananchi kesho kutwa Jumamosi, Agosti 6, huku watani zao Simba wakisherekea kilele cha Simba Day, Agosti 8 Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa utiaji msaada katika vituo viwili vya kulelea watoto yatima vya Islamic Hidaya kilichopo Olmatejoo na Huruma kilichopo Kiserian hapa jijini Arusa Mwenyekiti wa Yanga tawi hilo, Maulid Rashid amesema lengo kubwa ni kuwafikia wananchi na jamii kwa ujumla ili kutambua mchango wa timu hiyo.

Amesema pamoja na msaada huo, lakini bado wataendelea kushiriki shughuli zingine za kurudisha fadhila kwa jamii kwa kile walichokipata msimu uliopita ya kutwaa mataji yote tatu ya ligi,Ngao ya jamii,ubingwa wa Ligi na kombe la shirikisho la Azam Sports (ASFC).

"Hii imekuwa ni desturi yetu Wana Yanga na ndio maana timu yetu ina barikiwa kikubwa niwaombe matawi mengine nchi nzima wafanye hiki ambacho tumekifanya na sisi" amesema Rashid.

Katibu wa tawi hilo,Shabir Miraji amesema kutokana na usajili wa timu hiyo msimu kama mashabiki wanapongeza sana uongozi wao chini ya Rais Eng.Hersi Said ambaye amehakikisha vyuma vya maana vinasajiliwa.

Advertisement

Shabiki mwingine wa timu hiyo,Eliza Mwita amesema anafurahia kuona wanasiriki shughuli za kusaidia jamii kwani kwa kufanya hivyo njia ya ushindi imekuwa ikifunguka kwa timu yao kwani wengi wamekuwa wakiiombea mema.

Kuhusu usajili wao amesema wanachosubiri ni kuona ligi inaanza hili waanze kukusanya makombe yao huku akiwataka wapinzani wao kutegemea maumivu tu Ligi ikianza.

Akizungumzia msaada kutoka kwa mashabiki wa Yanga, mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Huruma,Yohana Msomba ameshukuru na kuwataka mashabiki wengine nao kuweza kujitokeza hili kuwapiga jeki katika kuwaudumia watoto hao.

Wiki ya Wananchi itaitimishwa kitaifa Jumamosi hii katika uwanja wa Taifa Dar ambapo Yanga itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Vipers SC kutoka nchini Uganda.

Advertisement