Waziri Amina atuliza kimanzi

WAZIRI wa michezo Balozi, Amina Mohammed kamtaka kocha wa Harambee Stars, Francis Kimanzi asipaniki kuhusu maandalizi ta timu hiyo ya taifa kuelekea mchuano wake wa kufuzu ushiriki wa dimba la Afcon 2022.

Stars ina mechi ngumu dhidi ya Comoros hapo Novemba na mpaka sasa hawajaanza maandalizi.

Tayari Shirikisho la soka nchini FKF limefanikiwa kupata mechi ya kirafiki na Zambia lakini sasa ngori iliyopo ni kwamba serikali bado imekazia michezo kurejelewa kwa kuhofya tishio la kuzuka kwa janga la corona.

Wiki iliyopita Kimanzi alielezea wasi wasi wake kuhusiana na namna serikali inavyojitokokota kuruhusu michezi irudi.

Kimanzi alihoji ili Stars kuwa na maandalizi mazuri ni lazima ianza vikao vya mazoezi mara moja lau sivyo itakuwa ni kupotea muda kucheza mechi ya kirafiki kabla ya kukutana na Comoros.

“Hatujacheza soka kwa miezi sita, hii ni hatari sana kwa mchezaji yeyote wa kulipwa kote duniani. Ikiwa tunalenga kufanya vizutri katika vibarua tulivyonavyo mbeleni basi ni lazima tuanze maandalizi mapema. Tunahitaji mwezi mzima wa maandalizi hivyo serikali inapaswa kufanya kitu, huku kukazia sio kuzuri” Kimanzi alipaniki.

Lakini sasa Waziti Mohammed kamjibu kwa kumtaka aache kupaniki huku akimhahidi kuwa ataanza maandalzi ya timu yake mapema.

“Jamani sielewi ni kwa nini watu wanatulaumu sisi kwa sababu maelezo na maagizo tunayotoa tunafanya hivyo baada ya kupata ushauri kutoka Wizara ya Afya. Kuna sababu tumeruhusu baadhi ya michezo kurejelewa naamini hata hili tutalipatia suluhu hivi karibuni” Mohammed kasema.

Stars inahitaji alama tatu dhidi ya Comoros kwenye mechi ya nyumbani na ugenini ili kuwa na matumaini ya kufuzu kwa dimba hilo. Comoros kwa sasa wanaongoza kundi hilo kwa alama nne huku Stars wakiwa na mbili tu.