Wakimbiaji 200 waandhimisha wiki ya usafiri wa Anga Duniani

Mkuu wa Wilaya ya Ilala (katikati)Ngw'ilabuzu Ludigija  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya uasafiri ya Anga Tanzania TCAA Hamza Johari (wa pili kulia) wakiwa katika mbio hizo za kuadhimisha wiki ya usafiri wa Anga dunia

Muktasari:

Lengo la mbio hizo ilikuwa ni kuweka miili sawa na hasa ikizingatia maambukizi ya Covid yamewagusa na wao katika kuelekea kilele cha wiki ya usafiri wa Anga Duniani.

ZAIDI wa wakimbiaji 200 wameshiriki mbio za kujifurahisha 'fun run' katika kuelekea kilele Cha wiki ya usafiri wa Anga duniani ambayo ufanyika kila tarehe 7 Disemba.

Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imefanya (fun run) kwa ajili ya kuadhimisha kilele Cha wiki hiyo kwa kuweka miili yao sawa

Kutokana na athari ya kuenea kwa wimbi la Covid 19 Duniani ambalo limeathiri pia sekta hiyo ndiyo sababu kubwa ya mwaka huu kufanya mbio hizo zilizokuwa za km 10 na km 5 ambazo zilishirikisha na familia pia.

Akizungumza baada ya mbio hizo Mkurugenzi Mkuu TCAA, Hamza Johari amesema mwaka huu kilele chao watafanya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa vitanda 28 katika shule ya Azania iliyopo Dar es Salaam.

Amesema, mazoezi ni muhimu na ni moja ya kujenga afya kwa wafanyakazi huku akiwataka kuendelea kufanya hivyo baada ya kazi ili kuweka miili yao sawa.

"Wiki ya usafiri wa Anga Duniani ufanyika kila Disemba 7 ya kila mwaka, sisi tumeshiriki mbio hizo fupi na tumefurahi kwa kushirikiana na wenzetu wa Mamlaka ya viwanja vya ndege, Precision Air, Atcl pamoja na watu binafsi wamejumuika na sisi, "amesema.

Kwa upande wake Mgeni rasm katika mbio hizo Mkuu wa wilaya ya Ilala

Ngw'ilabuzu  Ludigija aliwapongeza TCAA kwa kufanya mbio hizo ambazo anaamini Ni moja ya sababu ya kujenga umoja kwao na kuwafanya kuwa fiti.

"Nimeungana nanyi kwa kuthamini michezo ni afya na nimekimbia km 5 nimefurahi kukutana na watu wengi na hii ni nzuri kwa sababu mtumishi anajiweka sawa nje ya kazi, "amesema Ludigija.