Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

WAFCON: Twiga Stars njia hii hapa

Muktasari:

  • Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kushiriki michuano hii baada ya mwaka 2010, fainali zilizofanyika Afrika Kusini na iliishia hatua ya makundi.

DROO ya mashindano ya mataifa ya Afrika kwa upande wa wanawake (Awcon), ilifanyika juzi usiku jijini Sale, Morocco na timu ya Taifa ya Tanzania imepangwa kundi ‘C’ lenye bingwa mtetezi Afrika Kusini, Ghana na Mali.

Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kushiriki michuano hii baada ya mwaka 2010, fainali zilizofanyika Afrika Kusini na iliishia hatua ya makundi.

Michuano ya mwakani inayotarajiwa kufanyika Morocco kuanzia Julai 05 hadi 26, Tanzania inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kupenya walau kutoka hatua ya makundi kwenda mtoano kutokana na mfumo ulivyo na wapinzani wake.

Michuano hii inayohusisha timu 12, zilizopangwa katika makundi manne, kila kundi lina nafasi ya kutoa timu tatu kwenda mtoano (robo fainali) na mbali ya washindi wawili wa juu, pia kunakuwa na nafasi ya upendeleo kwa timu mbili zitakazoshika nafasi ya tatu lakini kwa kuwa na takwimu nzuri.

Tanzania ina nafasi kwa sababu katika kundi lake ukiwaondoa Afrika Kusini ambao wanaonekana ndio wababe na bingwa mtetezi wa michuano hii,  Ghana na Mali kwa sasa hazionekani kuwa tishio sana.

Timu zote hizi hazijawahi kabisa kushinda kombe hili na zaidi Ghana ilishindwa pia hata kufuzu katika michuano iliyopita.

Wachezaji wa timu hii ambao wanaonekana kuwa ni mastaa kama Jacqueline Owusu anayecheza Real Sociedad hawapati nafasi ya kucheza katika timu zao kutokana na kushuka kwa viwango.

Hata hivyo, Ghana ndiyo timu ya pili katika kundi hili ambayo imepata mafanikio zaidi katika  michuano hii kwa kuishia nafasi ya tatu mara tatu na kucheza fainali tatu na mara ya mwisho kumaliza nafasi ya tatu ilikuwa mwaka 2016 michuano iliyofanyika Cameroon.

Kwa upande wa Mali pia mafanikio yao makubwa katika michuano hii ni kumaliza nafasi ya nne mwaka 2018 na kijumla imeshiriki michuano hii mara saba.

Hivi karibuni Tanzania iliwahi kucheza dhidi yao katika mchezo wa kirafiki uliomalizika kwa sare ya bao 2-2.

Mali pia kwa sasa haina mastaa wengi wanaocheza nje ya nchi yao na hata wanaocheza nje asilimia kubwa hawachezaji katika ligi kubwa.

Timu ina kundi la wachezaji wanaocheza Morocco, Aichata Sangare, Fanta Konate, Aicha Samake na Fanta Konate ambao ukimwondoa Samake anayecheza Sports Casablanca ambayo imekuwa timu tishio kwa wababe wa nchi hiyo ASFAR, waliobakia hawachezi katika timu zenye ushindani wa kuwania mataji kama ASFAR na Sports Casablanca.

Licha ya ugeni wao katika mashindano Tanzania inaweza kupenya hata kwa kupitia nafasi ya tatu kwenda mtoano ambako itakuwa imekaribia kuinua harufu ya kushiriki Kombe la Dunia kwani timu nne zitakazoingia nusu fainali huwa zinafuzu moja kwa moja kucheza michuano hiyo.


MAKUNDI MENGINE

Makundi mengine mawili yaliyobakia, kuanzia A ambalo linamjumuisha mwenyeji Morocco, Senegal, DR Congo na Zambia, mambo yanaonekana kuwa yatakuwa mazito kwani timu zote zilishiriki katika mashindano yaliyopita na kufanya vizuri.

Ukiondoa Morocco ambayo ilifika hadi fainali na kupoteza mbele ya Afrika ya Kusini, Senegal iliishia robo fainali na kupoteza mbele ya Zambia ambayo iliibuka mshindi wa tatu,

Hivyo raundi hii huenda wakahitaji kulipa kisasi kwa ilichofanyiwa mwaka jana.

Kwa upande wa DR Congo ambayo ilijiondoa katika hatua za kufuzu mara mbili katika mashindano ya mwaka 2016 na 2022, ni timu yenye historia nzuri kwani iliwahi kuibuka mshindi wa tatu katika mashindano ya mwaka 1998.

Kwenye michuano ya mwakani wanaonekana kuwa wataleta ushindani wa kutosha kwani wachezaji wao wa timu ya taifa ambao baadhi wanatokea TP Mazembe wameonyesha ubora mkubwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa upande wa Wanawake na jana walicheza fainali ya michuano hiyo dhidi ya ASFAR.

Hata hivyo, katika kundi hili hakuna hata timu moja iliyowahi kufanikiwa kuchukua ubingwa wa michuano hii.

Kundi B ambalo lina mabingwa wa kihistoria  Nigeria ambayo imeshinda kombe hili mara 11 ikiwa haijawahi kukosekana hata mara moja tangu mwaka 1991 ilipoanza kushiriki zaidi  nalo linaonekana kuwa la moto.

Nigeria ambayo  msimu uliopita iliishia nusu fainali baada ya kutolewa na Morocco msimu huu inaweza kutaka kurudisha ufalme wake kama ilivyokuwa mwaka 2014 baada ya kulikosa taji mwaka 2014.

Mbali ya kundi hili pia lina Tunisa, Algeria na Botswana ambazo zote zimewahi kushiriki michuano hii kwa zaidi ya mara moja.

Tunisia na Botswana zote zilikuwepo katika michuano iliyopita mwaka 2022 ambapo ziliishia hatua ya robo fainali.

Algeria haikushiriki mashindano yaliyopita, lakini pia ni moja kati ya timu zenye historia nzuri kwani imewai kushiriki mara tano na zote iliishia hatua ya makundi.