Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vumbi la kikapu kutimka kesho

Muktasari:

Yunsu ameiongoza Savio kukalia usukani wa  ligi hiyo ikiwa na pointi 22 amefanikiwa kufunga pointi 182 katika mechi 11 ambazo wamecheza hadi sasa wakati Imelda Hango akifikisha pointi 142 huku timu yake ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wakikusanya pointi saba na wamecheza mechi nne.

Dar es Salaam. Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA) inaendelea Jumamosi kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa.

Hadi sasa wachezaji kwa wanaume Sylvian Yunzu (Savio) na Imelda Hango (Vijana Queens) wakiendelea kung'ara kwa ufungaji.

Yunsu ameiongoza Savio kukalia usukani wa  ligi hiyo ikiwa na pointi 22 amefanikiwa kufunga pointi 182 katika mechi 11 ambazo wamecheza hadi sasa wakati Imelda Hango akifikisha pointi 142 huku timu yake ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wakikusanya pointi saba na wamecheza mechi nne.

Yunzu ameingia kwenye tano bora za wachezaji wanaoongoza kwa pointi akifuatiwa na Erick Lugora (Oilers) mwenye pointi 174, Mwalimu Kijogoo (Vijana) ana pointi 173, Ally Hashim (Ukonga Kings) pointi 165 na Amin Juma (Savio) pointi 161.

Yunzu ameingia katika wachezaji watano wanaoongoza kwa kutupia mitupo mitatu 'three point' akiwa ametupia pointi 43, Erick Lugora ana 23, Frnak Majura (ABC), Anthony Jeikanga (Vijana) na Jacob Marenga ambao wana pointi 17 kila mmoja, Ally Mnyamani (Savio) na Trofimo Chemundugwao (Magnet) nao wamegongana kwa pointi 16.

Wachezaji watano wanaoongoza kwa riboundi ni Frank Mwemezi (Mabibo Bullet) ana 109, Mwalimu Kijogoo (Vijana) amefikisha 88, Derick Elijah (Ukonga Kings) ana 81, Nelo Levene (Outsiders) amekusanya 76 na Amin Juma (Savio) amefikisha 75.

Kwa upande wa wanawake, waliongia tano bora wanaongozwa na Imelda Hango (Vijana Queens) amefikisha pointi 142, Faraja Mhoamiso (Jeshi Stars) ana 107, Lulu Masana (JKT Stars) pointi 94, Khadija Karambo (Vijana Queens) pointi 89 na Amina Ahmed (DB Lioness) ana pointi 71.

Khadija amewaongoza kwa mitupo 'three pointi' akiwa na pointi 14, Orlyne Londo wa DB Lioness amefikisha pointi tisa, Amina Ahmed (DB Lioness) ana pointi sita, Martha Mashaka naye kutoka BD Lioness amefikisha pointi tano pamoja na Imelda mwenye pointi nne.

Joyce Kaila wa JKT Stars anaongoza kwa ribound 64 akifuatiwa na Grace Thomas (Kurasini Divas) ana ridoundi 45, Leticia Mafwimbo (Oilers Princesses) amefikisha 41, Magreth Nicolous wa Vijana Queens wao wamepiga riboundi 38 pamoja na Jesca Ngisaise (Ukonga Queens) pointi 38.

Mechi zitakazochezwa leo ni nne Jeshi Stars atacheza na Tanzania Prisons Queens, Mgulani na Prisons, Jogoo dhidi ya Mabibo Bullet huku Oilers wakicheza na Ukonga Kings.